TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Kundi la waendesha pikipiki huko jimbo la Arizona Marekani liitwalo 'Bikers Against Child Abuse' ambalo huwaweka salama wahathiliwa wa unyanyasaji hasa watoto, ikiwa ni pamoja na kulinda nyumba zao usiku ikiwa mnyanyasaji hayupo gerezani.
Pia hawa jamaa huhudhuria mahakamani kushuhudia na kusikiliza kesi zilizotokana na madhara yaliyosababishiwa watoto, pamoja na kuwalinda ili wasilazimishwe au kuingia katika mtego wa kisheria.
Hawa jamaa walianza kwa kujitolea mtaani kwao ila wakajiongeza ili kuepusha unyanyasaji wa watoto na kuunda shirika la hisani la waendesha pikipiki.
Shirika linafanya kazi ya kulinda watoto katika nchi kumi na nane dhidi ya watu binafsi katika hali za hatari.
Kulingana na mmoja wa memba wa kundi hilo anasema, tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1995, mtaalamu wa tiba na mhudumu wa jamii John Paul Lilly, shirika lao "lipo kwa nia ya kuweka mazingira salama kwa watoto wanaonyanyaswa".
Haya nsugu zangu bodaboda someni hiyo!.