KERO Bodaboda kupiga mziki kwa sauti ya juu nyakati za usiku

KERO Bodaboda kupiga mziki kwa sauti ya juu nyakati za usiku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Natumani tunaendelea vizuri katika ujenzi wa Taifa letu, pia ningependa kuwapa pole wale wote waliofikwa na maafa na watanzania wenzangu kwa ujumla kwa tukio la kuporomoka kwa jengo maeneo ya kariakoo.

Moja kwa moja niende kwenye lengo la kuandika uzi huu;
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya madereva bodaboda kufungulia mziki wa redio zao ambazo zipo kwenye pikipiki hizo kwa sauti ya juu sana bila kujali nyakati.

Hasa huku kwetu uswahilini ndo balaa mpaka saa nane za usiku utaskia kelele hizo.

Sikatazi bodaboda kufungulia mziki huo na hata nikiwakataza neno langu sio sheria ila ningeziomba mamlaka zinazohusika kupiangalia hili suala mana sasa imekuwa kero kwa nyakati za usiku.

Ninaomba angalau wangewekewa sheria inapofika saa 6 iwe mwisho wa bodaboda hao kufungulia radio zao kwa sauti za kukera.

Sidhani hili jambo unaweza ukakutana nalo ukiishi maeneo kama ya Masaki.

Mwisho na hitimisha kwa kuomba mamlaka zinazohusika kujaribu kuliangalia hili jambo.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom