Sio rahisi kukielewa alichosema Lema kama hutotumia mlango wa sita wa fahamu au jicho la tatu kukitafakari kwa makini lakini yote kwa yote bodaboda wamefedheshwa sana.
Mwenye kulaani na kubariki ni Mungu pekee na mafundisho ya kiimani yanafundisha juu ya kuongezewa kwa kile ulichonacho. Bodaboda ni kazi ambayo Mungu anambariki mwenye nayo na mwanadamu kumlaani mwenye kuifanya ni kuonesha mipango ovu mtu aliyonayo kwa sababu binafsi.
MTAZAMO WANGU
Binafsi ninaamini maneno ya Lema juu ya bodaboda ni mkakati wa CHADEMA na sio maneno tu kwa sababu bodaboda ni kundi linaloiamini sana CCM na kwa jicho la tatu unaona Kuna mpango wa kulifarakanisha kundi hili na CCM ili CCM ikose ushawishi nawaombia mtashindwa na hamtoweza. Jicho la tatu linaona sio bodaboda tu wanaolengwa na CHADEMA baada ya hapa watakuja kwa machinga, mama ntilie n.k
Kwangu, hii ni agenda ya upinzani kuwafitinisha Wananchi. Wanalenga makundi makubwa na yenye ushawishi kwa CCM. Hakuna mtu timamu mwenye kuweza kuilaani kazi na shughuli halali ya mtu from nowhere bila Jambo kuwa na faida kwake.
USHAURI KWA BODABODA
Poleni sana kwa dhihaka kubwa mliyopewa na CHADEMA ninatambua hawaoni umuhimu wote na Mara nyingine mnatumiwa kwenye shughuli zao bila kulipwa na hii ni kuwadharau sana.
Msilie wala msilalamike CCM ni chama kinachowajali na kuwaheshimisha. Toka serikali ya awamu ya nne mpaka CCM ipo pamoja na bodaboda.
Tumieni umoja wenu kuwaonesha wale wanaowadharau na kushindwa kuona umuhimu wenu ninyi ni jeshi kubwa. Pia, ninawashauri muendelee kujirasimisha na kuunda umoja wenye kwa ajili yenu.
USHAURI KWA CCM
Kwa kuwa kile CHADEMA kimeona vijana hawa hawafai , hii kwenu ni fursa ya kuwajengea imani juu ya CCM. Wahakikishieni shughuli zao ni baraka na sio laana. Wawezesheni kwa mafunzo ya usalama barabarani na utumiaji salama vyombo vyao ,wahimizeni kujirasimisha na mwisho shirikianeni nao kwenye mipango ya maendeleo.
Kazi ni kipimo Cha utu ni Imani ya CCM.
Ni Mtetezi wa bodaboda na machinga