Bodaboda msilie wala kuumia, CHADEMA haioni umuhimu wenu lakini CCM inawajali na kuwaheshimisha

Acha uongo wewe! Eti vijana wanafuraha na bodaboda!
Kama ni kazi na ni nzuri namna hiyo mbona viongozi wenu au yeyote mwenye maisha mazuri hata kidogo tuu hampi boda mwanae afanye kazi hiyo ya furaha?
 
Kama unaona bodaboda in kazi wanunulie watoto wako waendeshe
 
Kwani hizo bodabboda walipewa na chama gani, tuanzie hapo
 
Umesahau namba ya simu sister
 
Propaganda hizi Western media
 
CCM ingekuwa inawajali hata WATOTO WAO wangekuwa WANAENDESHA BODABODA BAJAJI MACHINGA NA MAMA NTILIE Lakini Watoto Wao wako BANK KUU TRA BANDARI N.K
 
Viwanda vile laki tatu vilivyosemwa na waziri wa viwanda wa wakati huo eti vya kufyatua tofali na cherehani mbili ndivyo unavyokumbushia?
BAVICHA hamueleweki mjue mnasikitisha sana mnachanganywa sana na viongozi wenu. Kipindi viwanda vinajengwa mlipinga ujenzi wa viwanda leo mnasema viwanda vijengwe.
 
Zungumzia vijana wasio wasomi wanasaidiwa vipi kwenye ajira rasmi ?kwa vijana wasomi kila siku serikali inatengeneza mazingira ya kuwaajiri lakini vipi wale wasio wasomi ambalo ni kundi kubwa zaidi.
Ninyi ndiyo wale wasomi mliopewa dhamana ya kuishauri serikali lakini mnashindwa kuleta tija. Hivi hapo kuna kazi ya kuumiza kichwa kuwaandalia ajira salama vijana wasio na elimu? Haya pamoja na kuwa sina elimu kubwa nakupa mfano.

Chukua vijana waliosoma wagawe ktk makundi ya vijana wanne wanne na wakasambazwe ktk maeneo yenye rutuba wakiwaongoza vijana wasio na elimu wapatao 100 kwa kila sehemu yenye rutuba huko shambani ambako serikali itawawezesha pembejeo na masoko. Fahamu kuwa tunayo maeneo mengi yanayofaa kwa kilimo cha mvua na umwagiliaji pia. Ufuatiliaji na usimamizi uwe chini ya wizara je hapo ni vijana wangapi wataajiiwa kama si zaidi ya milioni ktk ajira salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…