Baadhi ya waendesha pikipiki Jijini Dar es Salaam wameomba kuambatanishwa kwenye ziara za Rais Samia Suluhu Hassan anazozifanya nje ya nchi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao.
Maombi hayo yametolewa hivi karibuni katika kikao cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dar es Salaam ambapo bodaboda hao wameomba kuambatanishwa kwenye ziara hizo kwa ajili ya kukutana na kampuni za kutengeneza pikipiki ili wapate teknolojia bora.
Wamesema teknolojia hizo zitawasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa pikipiki wakitoa mfano kuwa nchini India kuna bajaji zinazotumia nishati ya gesi hivyo wakipata nafasi ya kuzungumza na watengenezaji wa bajaji hizo zitawasaidia kupunguza gharama.
Pia Soma:
-
Rais Samia kuanza kusafiri na Wasanii kwenye ziara zake nje ya nchi