Bodaboda Tabora tunaishi kwa wasiwasi na hofu ya kuuwawa

Bodaboda Tabora tunaishi kwa wasiwasi na hofu ya kuuwawa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kufuatia kuripotiwa kwa matukio ya kuuawa na kuporwa kwa pikipiki za maafisa usafirishaji (bodaboda) mkoani Tabora, Umoja wa Maafisa hao (UMUTA) mkoani humo umelaani vitendo hivyo huku wakiviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Usafirishaji Mkoa wa Tabora, Mrisho Shime, amesema kuwa wamejipanga kushirikiana kwa karibu na vyombo vya usalama ili kuhakikisha matukio hayo yanakomeshwa kabisa.

Aidha, ameeleza kuwa kwa mujibu wa uchunguzi walioufanya, matukio hayo yamekuwa yakijitokeza zaidi nyakati za katikati ya mwezi. Kutokana na hali hiyo, ametoa wito kwa wananchi kuwa wazalendo kwa kufanya shughuli halali za kujiingizia kipato na kuachana na njia haramu za wizi na ukatili.


 
1. Shida ya tabora, bunduki za jadi zipo nyingi sana, na muingiliano wa watu waovu ni mkubwa sana.

2. Vijana hawataki kufanya kazi ngumu, wanapenda mteremko balaa, ukiwa na pesa kuwamiliki wanyamwezi ni simple sana.

3. Vijana wa tabora, nilikuwa nawanunulia bangi ndoo zima kisha nawakabidhi, niliishi kama mfalme, mda wote nilikuwa natembea. 😁😁
 
Mtu ananunua tvs mpya anasanya hadi saa 7 usiku.... Wanaomkaba na kumuibia na hata kumuua ni hao hao bodaboda wenzake..... Hasa wanamuua wakigundua amewajua au amejua mmoja
 
Back
Top Bottom