Bodaboda uliyekwapua simu yangu maeneo ya Urafiki ukatubu la sivyo kifo chako hakiko mbali

Bodaboda uliyekwapua simu yangu maeneo ya Urafiki ukatubu la sivyo kifo chako hakiko mbali

Yaleyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
1,797
Reaction score
2,410
Wasalaam wana JF.
Leo nimekwapuliwa simu na bodaboda maeneo ya urafiki karibu na stendi ya Kilimanjaro Express.
Issue ilikuwa hivi. Nilikwenda kupokea mgeni wangu hapo stendi mida ya saa 3 usiku huu. Katika kuwasiliana na mgeni wangu kumbe bodaboda kanilia mingo. Nimeshtukia simu imekwapuliwa huku namwona mwizi wangu akitokomea.

Nilikuwa na manati ya mzungu lakini nilisita kuitumia. Huruma ya ghafla ilinishika baada ya kuona wewe bado ni kijana mdogo na kwa vyovyote unategemewa na wazazi wako au hata mke na mtoto. Kwa umbali uliokwepo nisingekukosa.

Kwa nini una risk maisha kiasi hicho wakati una bodaboda inayokuingizia kipato halali? Yawezekana haupo JF lakini naamini watu wenye tabia kama hiyo walioko JF watapata funzo.

Simu yangu imeniuma lakini niliona uhai wako ni muhimu kuliko hiyo simu.
 
mkuu umetumia sim gani kupost hapa, hata hivyo umefanya vizuri kutotumia hiyo manati, hao madogo wengi ni wezi wa temeke, cha muhim kama una imei za hiyo sim itrace utamshika kama kuku, kuna mmoja alifwatwa hadi mlangoni aliiba sim ya afisa galaxy s10 mamaer alijuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna jeuri ya kuhit moving object kwa manati ya mzungu,huo ndio ukweli,kwanza ukikwapuliwa kuna sekundi kama 15 to 20 za mshangao,wakati wewe unashangaa bodaboda inachanja mbuga kuwiden gap,labda umepiga warning shot lakini sio kumpata mwizi wako
 
Ungelenga boda boda tu.... au ulisahau kama unayo!...hongera kwa roho nzuri kama uliikumbuka ukaacha kumpiga.
 
hili tukio kama ukifanikiwa kuliripoti Police Post...kwa kadiri ninavyojua..

~kwanza lazima unyanganywe hiyo Pistol
~Pili,ukimkuta Afande Marwa yuko shift lazima akusweke locapu...hata Afande Bula anakuswaga

*pia kumbuka kauli ya Mkuu wa Kaya...watu kama hao ni "lazima uwalaze chini taratibu" kwa hiyo ume - fail

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikihurumie kiumbe usichokizaa mkuu[emoji124][emoji124][emoji124]

Sent using OPPO Mobile Phone
 
Soma vizuri maelezo, siyo unakuja na maswali ya kipuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimesoma haya maelezo vizuri nimeyaelewa Bodaboda uliyekwapua simu yangu maeneo ya Urafiki ukatubu la sivyo kifo chako hakiko mbali.
Gari yako uliuza au bado ipo gereji?
 
Hongera kwa kuibiwa mkuu,wewe ulikuwa na simu mbili na manati ya mzungu wenzako hata kitochi hawana....halafu bodaboda wa jf hawana tabia hizo wanamiliki boda za kutembelea ni matajiri kama wewe.
 
Huna jeuri ya kuhit moving object kwa manati ya mzungu,huo ndio ukweli,kwanza ukikwapuliwa kuna sekundi kama 15 to 20 za mshangao,wakati wewe unashangaa bodaboda inachanja mbuga kuwiden gap,labda umepiga warning shot lakini sio kumpata mwizi wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulichokisema ndo cha kweli na hakika mkuu.

Wengi wetu hubeba silaha kama mapambo ya kutishia warembo na hawana uwezo wa kuzitumia hata waingizwe kwenye mitego ya kuondolewa uhai wao wenyewe!

Mara ngapi tumeshuhudia mtu anafanyiwa ujambazi wa kinyang'au kabisa, bastola mkononi huku akitetemeka kama igizo la r.i.p Majuto la godoro la Confy!

Hatuzifanyii mazoezi kutuwezesha kujilinda nazo ama kupambana na adui wa ghafla kama ilivyotokea kwa mtoa mada.

Angeingia kwenye anga zang, huyo kibaka angelinyea mikononi mwangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom