Bodaboda wamegeuka kuwa wezi na vibaka

Bodaboda wamegeuka kuwa wezi na vibaka

Mkuu kweny msafara wa mamba na kenge wamo, sio sahihi na sawa kuamua kuwatusi bodaboda wote kwa kosa au mapungufu ya watu wachache mi navojua hao unaowaita wezi sio bodaboda bali ni wezi na vibaka wanaiba kwa kutumia pikipiki maana sisi bodaboda wenyewe tunaipenda na kuiheshimu kazi yetu.
Hicho kitu Ni kweli na naamini bodaboda walio wengi wanaofanya kazi hii mda mrefu niwastaarabu na Hao Hao huwakomesha Hawa vibaka wa kisingizio cha bodaboda sababu huharibu taswira nzima ya bodaboda..
 
Naunga mkono hoja
Kuna swali unaulizwa na wadau ili wajifunze kitu lakini unalikwepa.

Je Hiyo Bodaboda alipandia Kijiweni au ilikua inapita barabarani mkasimamisha? Na kama ni kijiweni je ni kijiwe gani ili watu wakikwepe wanapokua maeneo hayo?

Asante
 
Kuna sehemu tulienda, kurudi ilibidi nimuache sehemu alipohitaji Mimi nikaendelea na safari zingine. Alikuwa mbali kidogo na ulingo wa maeneo ya nyumbani
Mwambie asiwe anapanda bodaboda au bajaji kabla hajanote namba, hasa usiku na kuzituma kwa mtu wa karibu,, na huyo boda ajue wazi kuwa amenote namba
 
Bodaboda ni wezi sana. Kuna kisa nilisikia wanavizia magari yakiwa yanasubiri kuingia getini majumbani hasa mida ya usiku wanavamia. Kama hujalock mlango au kupandisha vioo imekula kwako.
Hakuna sehemu ya hatari kama kwenye geti ama mlangoni kwako,
Inashauliwa unaporudi kwake macho yako yaaangalie angle zote kwa makini,
Getini kwako ndo mtu hata kama amekukosa kukupata sehemu zote, anajua kwako lazima urudi,,
Hivyo unaporudi kwako na unasubiri geti kufungulia macho yake yatakiwa kuwa busy mda wote
 
Hakuna sehemu ya hatari kama kwenye geti ama mlangoni kwako,
Inashauliwa unaporudi kwake macho yako yaaangalie angle zote kwa makini,
Getini kwako ndo mtu hata kama amekukosa kukupata sehemu zote, anajua kwako lazima urudi,,
Hivyo unaporudi kwako na unasubiri geti kufungulia macho yake yatakiwa kuwa busy mda wote
Kuna video clip nliiona ya huko nje. Huyo mama aliingiza gari ndan mara kwa nyuma wakatokea wazee wa kazi na gari nyingine wakablock gate wakashuka na bastola wanamtishia afungue mlango. Yule mama alichofanya akarudi nyuma akaigonga ile gari ya majambazi. Wale watu walipigwa na butwaa na mama huyo akakazana kuigonga. Wale wezi wakakimbia wakaacha gari yao
 
Haya makundi ya bodaboda yaangaziwe kwa jicho lingine kabisa kwa watumiaji wake.

Baadhi yao ni vibaka, wezi na wanyang'anyi..

Wamemkaba wife Leo mda mchache baada ya kuachana nae, bodaboda aliyemkodi ndie aliyemkaba huko njiani na kumnyang'anya pochi iliyokuwa na simu, pesa pamoja na document kadhaaa.

Ni bora hata wangechukua pesa na simu wakaacha hizo document. Hii mijinga ndio maana huwa inachomwa moto.

Pumbavu kabisa.
Usikodishe bodaboda njiani,barabarani,kusiko na kituo Chao.Kodisha kwenye kituo Chao na hakikisha ni wa hapo,ndio maana vituo vya bodaboda,bajaji,Taxi,hawaruhusu kupaki hapo,kama hajasajiliwa na kujulikana,kwenye kituo Chao.Ukiibiwa au ukisahau kitu,unafatilia kwenye kituo Chao,na utamkuta au ukiulizia wenzake,watakupa taarifa zake.Au kodisha bodaboda,bajaj ,Taxi za uber,linkee,bolt,taxify
nk.Ambazo zipo playstore,hawezi kukuibia,kwasababu unamkodisha kwa application,yenye jina la dereva na namba za simu,na ofisini kwao,anajulikana.
 
Haya makundi ya bodaboda yaangaziwe kwa jicho lingine kabisa kwa watumiaji wake.

Baadhi yao ni vibaka, wezi na wanyang'anyi..

Wamemkaba wife Leo mda mchache baada ya kuachana nae, bodaboda aliyemkodi ndie aliyemkaba huko njiani na kumnyang'anya pochi iliyokuwa na simu, pesa pamoja na document kadhaaa.

Ni bora hata wangechukua pesa na simu wakaacha hizo document. Hii mijinga ndio maana huwa inachomwa moto.

Pumbavu kabisa.
Chukua uber, bolt na kama hizo au unaye mfahamu
 
Mbona unaweza kukodish bodaboda,bajaj,Taxi za bolt,uber,linkee,taxify
Na bei ni za kawaida.Hawa unatumia app.yao unawapata bila tabu.Ukisahau kitu kwao,unapiga simu ofisini kwao,wanamtafuta,unapata ulichosahau.
 
Kwa Wakuu wala bata.
Tuweke mambo wazi. Hali hivi sasa hali ni mbaya sana. Vijana ni wengi mno mitaani, acha wale ambao wako kwenye foleni ya kuingia mitaani!(pitia shule za msingi asubuhi wakiwa Assembly).
Mambo ya kufanya:
Acha starehe za hovyohovyo, wahi nyumbani.
Usipende lifti hovyohovyo!
Kama huna shughuli maalum ya kukutoa nje, kaa nyumbani kwako.
Ikiwezekana, hakikisha wewe na familia yako saa moja jioni mko nyumbani.
Uwe na bodaboda, bajaji, taxi, maalum. Hata kama uko mbali mpigie simu akufuate. Jali usalama, usihurumie pesa.
 
Pole sana, mue mnaangalia na zakupanda, unaona jitu huni kabisa na bado unapanda boda boda yake...
 
BIASHARA YA BODABODA IRATIBIWE, HII ITAPUNGUZA FURSA YA UHALIFU :

  • Halmashauri isitishe utitiri ukiopitiliza wa bodaboda
  • Halmshauri ikadirie wilaya yake inahitaji bodaboda ngapi na isiruhusu kutoa leseni bila kikomo
  • Halmashauri iweke kiwango cha kodi kwa bodaboda, anayeshindwa anyanganywe leseni
  • Kuwepo chama thabiti cha wale wafanyabiashara wa bodaboda na wazuie wingi uliopitiliza wa wanachama.
  • Kila muendesha bodaboda avae vazi rasmi linaloonesha namba ya kijiwe na sehemu leseni iliposajiliwa
  • Mwisho kwa Kila mwendesha pikipiki lazima aeleweke ana shughuli gani atembee na kitambulisho rasmi, kama ni mlipakodi wa huduma za kusafirisha parcels, vyakula n.k ijulikane
 
Msiwe na mawazo pindishi mda wote.

Hili jizi mpaka mda huu linatumia simu hiyo kutapeli watu kupitia namba zilizopo kwenye simu. Kwa kutuma ujumbe wa kitapeli..

Sema police kitengo cha cyber hamna kitu angekuwa ashakamatwa huyu
Polee msaidie hiyo simu waifunge. Ndugu wataibiwa sana wakijua ni mkeo.
 
Back
Top Bottom