Bodaboda wamtuma Mjema kwa Rais Samia

Bodaboda wamtuma Mjema kwa Rais Samia

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
BODABODA WAMTUMA MJEMA KWA SAMIA

VIONGOZI wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda Tanzania, leo Agosti 9, 2023 wamefika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam na kuzungumza na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Ndg. Sophia Mjema.

Viongozi hao walimuomba Ndg. Mjema kumfikishia salamu za pongezi Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoongoza nchi na kutatua kero zinazowakabili wananchi wa makundi mbalimbali wakiwemo wao.

Walimtuma Ndg. Mjema amweleze Rais Dkt. Samia kwamba wanamuunga mkono katika kazi anazofanya kuhakikisha nchi inapata maendeleo na maisha ya Watanzania yanakuwa bora.

Kwa upande wake Ndg. Mjema aliahidi kuzifikisha salamu hizo na kuwashukuru kwa kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi.

IMG-20230810-WA0001.jpg
IMG-20230810-WA0002.jpg
IMG-20230810-WA0004.jpg
IMG-20230810-WA0005.jpg
IMG-20230810-WA0007.jpg
IMG-20230810-WA0006.jpg
 
[emoji23] Mimi ni boda boda wapi tumeungana kupeleka pongezi.
Yani mnajiingiza vidole na kunusa kujua upepo hupo wapi.
Mtatafuta mpaka kiongozi wa panya road kuja kupongeza
 
Back
Top Bottom