Bodaboda zinajenga uchumi au zinadidimiza uchumi?

Mbekenga

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2010
Posts
3,262
Reaction score
8,144
Ili kuongeza thamani ya Shilingi, inabidi tuzalishe (kwa kulima, kusindika) kwa ajili ya matumizi ya ndani na ziada kwa ajili ya mauzo ya nje. Sasa hawa wazungu (wachina) wameona ili tubaki tegemezi wanaamua kuzalisha na kutuletea na kuteka akili za vijana badala ya kwenda kuzalisha wao wanakimbilia kuendesha bodaboda.

Hasara
-Kutengeneza vikundi vya vijana wanaopanga uharifu vijiweni wakati wakishindania abiria
-Mfumuko wa bei utokanao na vijana wengi kutozalisha
-Mfumuko wa bei utokanao na wananchi kuingia gharama kubwa kulipia usafiri (safari unayolipia sh.300 kwa daladala utalipa sh. 3000 kwa bodaboda.

kama nimekosea basi nikosoe hayi ni mawazo yangu juu ya wazungu wanavyochezea akili yetu
 
Zinajenga uchumi coz mahali ambapo ulikuwa unatumia four hours to reach now you use one hour or less.
 
Swala sio kwa nini kuwe na boda boda etc. serikali ambayo mosi imeshindwa kusimamia njia kuu za uchumi wake itaendelea kuwa tegemezi. Huwezi leo hii kuwa nchi huru wakati njia kuu za uchumi zinamilikiwa na wachache. Kama serikali inataka hii nchi isonge mbele ni lazima njia kuu zote za uchumi zimilikiwe na serikali. Hata nchi zilizoendelea zote hakuna watu wachache wanaomiliki njia zake za uchumi.

Tumekuwa taifa la wendawazimu, viongozi wetu wamewaachia watu wachache kutupigisha gwaride ambalo linawaneemesha mafisadi.
 
Katika kila jambo kuna pande mbili mkuu, upande chanya na upande hasi, sasa uzito ukiwa mkubwa upande hasi jambo hilo huwa ni hasara kwa jamii husika na kinyume chake kinahusika. Nitakupa mfano mdogo, mimi nikitoka Dar kwa bus inabidi nishuke njiani na inabidi nilale pale mpaka kesho ( zamani kabla ya boda boda),sasa hivi silali pale, nashuka kwenye bus, naingia kijijini na kugeuza siku hiyo hiyo kuja kusubiri bus asubuhi,kwa hiyo safari ya siku nne sasa ni siku mbili tu. Kwa hiyo naweza kuzusha ED kazini na nikafika home na kurudi bila zengwe.Nimeokoa muda na fedha.

Boda boda hiyo hiyo inapowafanya vijana wakae vijiweni bila kazi ni mbaya, au ikitumika kumpeleka jambazi kwenye uhalifu. Kwa ufupi ni kwamba, ikitumika vizuri na kwa nidhamu, boda boda ni nzuri.
 
zinavunja uchumi na zinavunja miguu ya watumiaji pia. ukitaka kuhakikisha nenda MOI.
 
Mkuu sijui labda ni kwa nini umeamua kutumia kipimo cha boda boda kua ndio kinaua uzalishaji.
Labda hukuangalia pato serikali inaloingiza kwa kodi ya hivi vyombo vya moto, na labda ufanisi wa muda katika safari zilizokua zinachukua siku nzima leo ni masaa tu.
 
zinavunja uchumi na zinavunja miguu ya watumiaji pia. ukitaka kuhakikisha nenda MOI.

Zinavunja uchumi kivipi? Na zinavunja miguu kivipi? Suala la ajali lipo siku zote hata kabla ya boda boda. Uzembe wetu ktk sheria ndio uliopelekea miguu kuvunjika. Tuzungumzie boda boda kama ikitumika kama ilivyo kusudiwa mkuu. Au angalia mfano wa pili unaofanana na huo ni huu, kasimu kangu kenye line ya voda kanapopeleka hela kijijini kwa mjomba ndani ya sekunde kanakuwa kameokoa muda na gharama zaidi, lakini kasimu hako hako nikikatumia kutukana mtu au kuwasiliana na wezi ili waibe ofisini kwetu,hapo kipi kitakuwa ni kibaya, simu au mimi mtumiaji?

Kwa hiyo utaona kwamba, boda boda kama ilivyo haina neno, neno lipo kwetu watumiaji. Je unaitumia positively?
 
Kwa kifupi ni Kwamba zinakuza Uchumi wa China na si Tanzania, sasa zikikuza Uchumi wa Tanzania na huko zinako Tengenezwa itakuwa Vipi? Japani iko pale ilipo kwa sababu ya Kuuza sana Toyota nje ya nchi yao, na Toyota inakuza Uchumi wa Japani na si vinginevyo,

Hapa Tatizo liko kwa Upande wa Serikali yetu make wale vijana wameamua kujiajiri baada ya kuwa Viwanda vyote vimeuwawa na vilivyopo ni Vidogo vidogo vinavyo chukua watu wachache, laiti kama Kungekuwa na Viwanda vya Kutosha mambo ya kuendesha Bodaboda yasingekuwepo,

Ili nchi isonge mbele ni lazima ilazailishe kwa wingi sana na kuuza nje ya Nchi hapo ndo kukuza Uchumi, sasa Bongo Tunadanganyana na Dhahabu, Mara Tanzanite, Mara alumasi, mara sijui makaa ya mawe, haya Madini kwanza makaa ya mawe kwa sasa ni nchi chache sana wanatumia, Ulaya walisha achana nayo long tim,e make techinolijia ya kuyatumia ni ya Long sana,

Na kwa ujumla hakuna nchi iliyo endelea kwa Madini, nchi kama Austrarila wana Chimba madini ya Kufa mtu lakini kinachoe inyayua ni viwanda na si Madini, South Africa wanazalisha sana Madini but Viwanda ndo vinaifanya South Africa iwe pale ilipo kwa sasa,

So Tanzania tunacho fanya Ni kukuza Uchumi wa Mataifa kama China, India na kwingineko kwa sababu sisi ni soko la hizo bidhaa, Ishu kwamba Bodaboda zinalipa Kodi halina Mantiki kabisa, basi Nchi kama Japan inayo uza magari kwa wingi sana yangekuwa yanakuza Uchumi wa Hizo nchi zinazo nunua kupitia Kodi,

Kilichopo ni nchi kuwekeza katika Viwanda, kama hata Touthpiki tunaagiza wewe unategemea nini? Tunaagiza hadi Toilet Paper, halafu useme kwa sababu tunalipa Kodi basi tunakuza Uchumi wetu,

Nchi kama Kenya wao wako juu zaidi ya Tanzania kwa sababu ya Viwanda na si vinginevyo, sasa sisi tunazani tunaweza shindana na mataifa mengine kwa kuwa na Madini, kwanza tukumbuke Madini sio bidhaa muhimu ambazo ni lazima Nchi iwe nazo,

Only Viwanda ndo viatakvyo kuza Uchumi wa Nchi na si biashara ya Uchuuzi wa bidhaa za China, India na Ulaya
 
Hizo Boda boda zingekuza Uchumi wa Tanzania kama tunmgekuwa tuna Tengeneza wenyewe na kuzitumia na zingine kuuza Nje ya Nchi, hapa the more Toyo zinavyo agizwa Nje ndo the more kule China watu wanapata ajira, viwanda vinajitanua, Serikali ya China inapata Kodi na kazalika,

Siwezi kataa kwamba inarahisisha mawasiliana kutoka sehemu mohja kwenda nyinmgine, Ila kwa ukweli haziwezi kuza Uchumi kwa speed ya zinavyo kuwa wa Nchi zilipo toka,
 
Ili kuongeza thamani ya Shilingi, inabidi tuzalishe (kwa kulima, kusindika) kwa ajili ya matumizi ya ndani na ziada kwa ajili ya mauzo ya nje. Sasa hawa wazungu (wachina) wameona ili tubaki tegemezi wanaamua kuzalisha na kutuletea na kuteka akili za vijana badala ya kwenda kuzalisha wao wanakimbilia kuendesha bodaboda.

Hasara
-Kutengeneza vikundi vya vijana wanaopanga uharifu vijiweni wakati wakishindania abiria
-Mfumuko wa bei utokanao na vijana wengi kutozalisha
-Mfumuko wa bei utokanao na wananchi kuingia gharama kubwa kulipia usafiri (safari unayolipia sh.300 kwa daladala utalipa sh. 3000 kwa bodaboda.

kama nimekosea basi nikosoe hayi ni mawazo yangu juu ya wazungu wanavyochezea akili yetu

Mtizamo wangu ni tofauti sana na mtizamo wako! Unachukizwa na Wachina kutengeneza vitendea kazi rahisi! Inasemekana watu wasio na maendeleo wameelemea sana katika kulalamika! Kusingizia daima kuwa watu wengine wanahusika katika matatizo yao!

Ingawa imetokea kuwa baadhi ya vitu vya wachina havidumu lakini kwa hakika Africa na hasa watu wenye uwezo mdogo tunapaswa kuwashukuru sana wachina kwamba wamechochea sana kufanya watu wengi kushiriki kuzungusha gurudumu la maendeleo! Kabla ya hizi piki piki nyingi ambazo zimeleta msamiati wa BODABODA ni wachache sana walikuwa na uwezo wa kununua pikipiki za kijapan kama Honda, Yamaha, Kawasaki nk. Hata leo ni wachache wanaweza kuzinunua piki piki hizo zikiwa mpya! Baada ya kuanza kumiminika pikipiki hizo ambazo awali watu walidhania hazidumu na kuzibatiza kuwa YEBOYEBO watu wengi waliweza kuzinunua! Hadi leo zimechochea maendeleo kwa kiasi cha kutisha. Pikipiki hizo zinaweza kuingia maeneo ambayo barabara ni duni au hazipo, watu wanaweza sasa kufanya mambo mengi kwa siku moja kwa uharaka kuliko ilivyokuwa awali! Watu wengi wanapoweza kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa urahisi zaidi ni hatua kubwa ya maendeleo!

Wachina wanatengeneza mitambo mingi sana ya uzalishaji kwa bei nafuu ukilinganisha na nchi za Ulaya, America na Japan! Kama wewe huna ubunifu wa kutengeneza kitu cha kukuzalishia au kukurahisishia kazi, akatokea mbunifu akatengeneza vifaa hivyo kwa bei inayonunulika ni uhayawani kumchukia mtengenezaji huyo! Huyo mtengenezaji ni baraka kwa watumiaji! Wakati Africa tunalalamika na kulialia wenzetu nchi zote zinazoendelea na zilizoendelea ikiwamo USA bidhaa za China zinamiminika na watu wananufaika sana! Wachina wameshalishinda soko la dunia kwani wanajua mahitaji ya masikini na matajiri! Wazungu na Wamarekani na wajapan bidhaa zao daima zimekuwa zinalenga matajiri tu na hazijawahi kutusaidia lakini wachina wanajaza bidhaa zao kote kwa matajiri na masikini.

Kuhusu vijiwe, vijiwe ni tatizo pana sana la kisera na kisiasa! Vijiwe hivyo havisababishwi na BODABODA isipokuwa mtazamo wako ni wa wivu kuona BODA BODA zimezidi kuwa nyingi, hutambui kuwa kuna food-chain vijiweni ambapo bila hizo BODA BODA hali ya usalama ingekuwa mbaya zaidi mitani! Uzalishaji si lazima iwe viwandani pekee au mashambani tu bali hata huduma ni sehemu kubwa ya uzalishaji! Utalii, usafirishaji, mawasiliano, tiba na shule ni maeneo ya uzalishaji na ni huduma!

Wachina wanauza bidhaa na wanauza mitambo ya kuzalishia bidhaa! Hawajazuia sisi tusitengeneze mitambo yetu wala hawajazuia tusiinunue waliyoitengeneza wao ili tuweze kutengeneza bidhaa zetu wenyewe! Sisi hatuna uwezo wa kutengeneza mitambo, hatuoni haja ya kununua mitambo yao, hatuwezi kuzalisha na hata wakiuza mitambo kama hizo pikipiki WAAFRIKA kama desturi yetu tunaanza tena kulalama kwamba BODA BODA zinatudidimiza kiuchumi!

Nilizaliwa mwafrika nitakufa mwafrika lakini ninakiri waafrika tunatatizo kubwa sana kuna mapungufu vichwani. Moja ya sifa ya watu waliofeli duniani ni kulalamika na kuona matatizo yao yamesababishwa na watu wengine!

CHINA tawala dunia, CHINA tawala dunia ni wakati wako sasa!!
 
mi naona zinadumaza tu uchumi wetu. mfano bodaboda moja ikienda kilometa kumi na hiace yenye watu ishirini ikienda kilometa kumi mafuta yatakayo tumika kwa mtu mmoja kwenye bodaboda ni mengi sana kuliko yatakayo tumika na mtu mmoja kwenye hiace. pia haziwezi beba mzigo wa maana kwamba zisaidie usafirishaji wa kibiashara. watu wengi wanaopanda ni kwa shughuli binafsi na uvivu wa kutembea kitu kitakachopelekea kuwa na taifa la visukari na hypertension. kijana anakaa asubuhi mpaka jioni anapata 2500 kama pesa yake. ambayo ni sawa na 75000 kwa mwezi. akienda kulima au kuvua si atapata zaidi ya hapo!(usiniambie hawana mitaji).
 
Mkuu kwa kuwa una kazi na uhakika wa mlo usiwadharau hwa jamaa....hiyo nayo ni kazi kama kazi nyingine...
 
Mtizamo wangu ni tofauti sana na mtizamo wako! Unachukizwa na Wachina kutengeneza vitendea kazi rahisi! Inasemekana watu wasio na maendeleo wameelemea sana katika kulalamika! Kusingizia daima kuwa watu wengine wanahusika katika matatizo yao!

Ingawa imetokea kuwa baadhi ya vitu vya wachina havidumu lakini kwa hakika Africa na hasa watu wenye uwezo mdogo tunapaswa kuwashukuru sana wachina kwamba wamechochea sana kufanya watu wengi kushiriki kuzungusha gurudumu la maendeleo! Kabla ya hizi piki piki nyingi ambazo zimeleta msamiati wa BODABODA ni wachache sana walikuwa na uwezo wa kununua pikipiki za kijapan kama Honda, Yamaha, Kawasaki nk. Hata leo ni wachache wanaweza kuzinunua piki piki hizo zikiwa mpya! Baada ya kuanza kumiminika pikipiki hizo ambazo awali watu walidhania hazidumu na kuzibatiza kuwa YEBOYEBO watu wengi waliweza kuzinunua! Hadi leo zimechochea maendeleo kwa kiasi cha kutisha. Pikipiki hizo zinaweza kuingia maeneo ambayo barabara ni duni au hazipo, watu wanaweza sasa kufanya mambo mengi kwa siku moja kwa uharaka kuliko ilivyokuwa awali! Watu wengi wanapoweza kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa urahisi zaidi ni hatua kubwa ya maendeleo!

Wachina wanatengeneza mitambo mingi sana ya uzalishaji kwa bei nafuu ukilinganisha na nchi za Ulaya, America na Japan! Kama wewe huna ubunifu wa kutengeneza kitu cha kukuzalishia au kukurahisishia kazi, akatokea mbunifu akatengeneza vifaa hivyo kwa bei inayonunulika ni uhayawani kumchukia mtengenezaji huyo! Huyo mtengenezaji ni baraka kwa watumiaji! Wakati Africa tunalalamika na kulialia wenzetu nchi zote zinazoendelea na zilizoendelea ikiwamo USA bidhaa za China zinamiminika na watu wananufaika sana! Wachina wameshalishinda soko la dunia kwani wanajua mahitaji ya masikini na matajiri! Wazungu na Wamarekani na wajapan bidhaa zao daima zimekuwa zinalenga matajiri tu na hazijawahi kutusaidia lakini wachina wanajaza bidhaa zao kote kwa matajiri na masikini.

Kuhusu vijiwe, vijiwe ni tatizo pana sana la kisera na kisiasa! Vijiwe hivyo havisababishwi na BODABODA isipokuwa mtazamo wako ni wa wivu kuona BODA BODA zimezidi kuwa nyingi, hutambui kuwa kuna food-chain vijiweni ambapo bila hizo BODA BODA hali ya usalama ingekuwa mbaya zaidi mitani! Uzalishaji si lazima iwe viwandani pekee au mashambani tu bali hata huduma ni sehemu kubwa ya uzalishaji! Utalii, usafirishaji, mawasiliano, tiba na shule ni maeneo ya uzalishaji na ni huduma!

Wachina wanauza bidhaa na wanauza mitambo ya kuzalishia bidhaa! Hawajazuia sisi tusitengeneze mitambo yetu wala hawajazuia tusiinunue waliyoitengeneza wao ili tuweze kutengeneza bidhaa zetu wenyewe! Sisi hatuna uwezo wa kutengeneza mitambo, hatuoni haja ya kununua mitambo yao, hatuwezi kuzalisha na hata wakiuza mitambo kama hizo pikipiki WAAFRIKA kama desturi yetu tunaanza tena kulalama kwamba BODA BODA zinatudidimiza kiuchumi!

Nilizaliwa mwafrika nitakufa mwafrika lakini ninakiri waafrika tunatatizo kubwa sana kuna mapungufu vichwani. Moja ya sifa ya watu waliofeli duniani ni kulalamika na kuona matatizo yao yamesababishwa na watu wengine!

CHINA tawala dunia, CHINA tawala dunia ni wakati wako sasa!!

Mkuu Kubota, Nakushukuru saana, sina namna naweza toa shukrani zangu kwa mada yako japo ni kwa ufupii sana, pia nasikitika sana kuona maoni ya watanzania wenzetu mtazamo walionao hasa kwa kupitia mada hii, INASIKITISHA SANA,, Kwa ufupi mawasiliano ni moja ya sector nyeti sana katika kukuza uchumi wowote ule, kwa uhakita mojawapo ya usafiri ulioongeza speed ya uchumi hivi karibuni ni 1. BODABODA 2. FUSO,,,,,, Pia watanzania naungana na Kubota Tunapaswa kumshukuru sana mchina kwa namna nyingi sana,kwani kulingana na umasikini/uwezo wetu kupitia china tunapata uwezo mfano zana za kilimo- trectors, viwanda vidogovidogo na hata vikubwa, kuhamisha tecnologia kupitia china ni rahisi sana kuliko popote pale, infrastructures n.k.
 
Chasha umetoa elimu kwa wale waliochelewa kunielewa. Nilimaanisha kwamba badala ya kuzalisha tukauza nje sisi tunasubiri mchina afungue viwanda nchini kwake, atengeneze bidhaa, sisi tutumie au tumsaidie kuuza. Nakushukuru kwa kutoa elimu ya 'balance of trade'
 
Mheshimiwa au Ndugu KUBOTA nakupa cases mbili kama ifuatavyo:
1. Ukinunua mtambo wa kusaga nafaka kutoka China, utakuwa unalenga kukuza uchumi wa Tz kwa sababu badala ya kuajiri mtu mmoja (bodaboda driver), utaajiri watu wengi, utaongeza thamani ya mazao ya mkulima, utauza bidhaa nje ya nchi.

2. Ukinunua bidhaa ya china kwa ajiri ya kutumia (consumamble good) kama pikipiki utakuwa unakuza uchumi wa China, badala yake wewe au serikali ingewekeza kwenye utengenezaji wa pikipiki hapa nchini na kuajiri vijana
 
Katika kila jambo kuna pande mbili mkuu, upande chanya na upande hasi, sasa uzito ukiwa mkubwa upande hasi jambo hilo huwa ni hasara kwa jamii husika na kinyume chake kinahusika. Nitakupa mfano mdogo, mimi nikitoka Dar kwa bus inabidi nishuke njiani na inabidi nilale pale mpaka kesho ( zamani kabla ya boda boda),sasa hivi silali pale, nashuka kwenye bus, naingia kijijini na kugeuza siku hiyo hiyo kuja kusubiri bus asubuhi,kwa hiyo safari ya siku nne sasa ni siku mbili tu. Kwa hiyo naweza kuzusha ED kazini na nikafika home na kurudi bila zengwe.Nimeokoa muda na fedha.

Boda boda hiyo hiyo inapowafanya vijana wakae vijiweni bila kazi ni mbaya, au ikitumika kumpeleka jambazi kwenye uhalifu. Kwa ufupi ni kwamba, ikitumika vizuri na kwa nidhamu, boda boda ni nzuri.

boda boda ni nzuri sana. fasta ushafika town. serikali isaidie tu kuhakikisha tunaendeshwa na watu wenye leseni.
 
Mkuu Kubota, Nakushukuru saana, sina namna naweza toa shukrani zangu kwa mada yako japo ni kwa ufupii sana, pia nasikitika sana kuona maoni ya watanzania wenzetu mtazamo walionao hasa kwa kupitia mada hii, INASIKITISHA SANA,, Kwa ufupi mawasiliano ni moja ya sector nyeti sana katika kukuza uchumi wowote ule, kwa uhakita mojawapo ya usafiri ulioongeza speed ya uchumi hivi karibuni ni 1. BODABODA 2. FUSO,,,,,, Pia watanzania naungana na Kubota Tunapaswa kumshukuru sana mchina kwa namna nyingi sana,kwani kulingana na umasikini/uwezo wetu kupitia china tunapata uwezo mfano zana za kilimo- trectors, viwanda vidogovidogo na hata vikubwa, kuhamisha tecnologia kupitia china ni rahisi sana kuliko popote pale, infrastructures n.k.

Naona unaaply CIVICS kwenye maswala ya Uchumi, Unacho sema ni kweli kabisa, but Tanzania hatuwezi songa mbele kwa kuimport kila kitu, hakuna nchi iliyo wahi kuendelea kwa staili hii,

Nchi nyingi za Asia kama INDIA, CHINA, MALASIA, INDONESIA, KOREA, TAIWAN NA Zinginezo kwa sasa zimepiga hatua kutokana na kuwa na Viwanda vingi sana na wanatengeneza kila kitu na vitu vichache sana wana agiza kutoka nje,

Hata kama Boda boda zinarahisisha Mawasiliano zingetengenzwa Tanzania ndi ingekuwa vizuri, The more mnavyo nunua Bodaboda Nyingi ndo the More China inavyo zidi kujitanua kibiashara, wanaajiri watu wengi na pato linaongezeka,

Tatizo uchumi wa Bongo umejikita kuangalia faida za Mtu mmoja mmoja na si Nchi,

Techinolojia gani mmehamisha kutoka China? Taja moja tu, kwa mawazo yako unazani Kununua Vifaa vya China ndo kuhamisha Techinolojia?
 
Mheshimiwa au Ndugu KUBOTA nakupa cases mbili kama ifuatavyo:
1. Ukinunua mtambo wa kusaga nafaka kutoka China, utakuwa unalenga kukuza uchumi wa Tz kwa sababu badala ya kuajiri mtu mmoja (bodaboda driver), utaajiri watu wengi, utaongeza thamani ya mazao ya mkulima, utauza bidhaa nje ya nchi.

2. Ukinunua bidhaa ya china kwa ajiri ya kutumia (consumamble good) kama pikipiki utakuwa unakuza uchumi wa China, badala yake wewe au serikali ingewekeza kwenye utengenezaji wa pikipiki hapa nchini na kuajiri vijana
Nakubaliana na wewe Mbekenga, yawezekana tunaongea kitu kimoja kwa namna tofauti! Umekwenda mbali sana kulaumu hao wanaotuingizia mitambo na consumables. Umesahau kulaumu waliosababisha viwanda tulivyokuwa navyo tayari vikafa! Kama tunashindwa kusindika machungwa na nyanya zinazoozeana kila mwaka wewe unaota kiwanda cha pikipiki!? Thubutu! Wazungu (Wachina) walishaisoma na kuichambua sana akili yetu! Wanatujua udhaifu wetu sisi waafrika kuliko tunavyojijua wenyewe! Ninachotofautiana na wewe ni kudhani kuwa tatizo la ajira limesababishwa na wazungu siyo kweli! Labda kama unamaanisha kuwaWazungu walishacheza na akili yetu, wakipiga chenga tunapigika kirahisi, je ni hizo chenga tulizopigwa ndiyo zilitufanya tuibe na hatimaye kuua viwanda? basi wao wako juu, nadhani ni chenga hizo hizo tunapigwa toka enzi za Chifu Mangungo wa Msowelo hadi machifu wa leo! Mimi nadhani tatizo ni sisi wenyewe! Acha Wachina watuuzie toothpicks wakati tuna miiba mizuri maporini tungeikata tukauziana, mweee .......... walahi nabata uchungu!!
 
Mkuu Kubota, Nakushukuru saana, sina namna naweza toa shukrani zangu kwa mada yako japo ni kwa ufupii sana, pia nasikitika sana kuona maoni ya watanzania wenzetu mtazamo walionao hasa kwa kupitia mada hii, INASIKITISHA SANA,, Kwa ufupi mawasiliano ni moja ya sector nyeti sana katika kukuza uchumi wowote ule, kwa uhakita mojawapo ya usafiri ulioongeza speed ya uchumi hivi karibuni ni 1. BODABODA 2. FUSO,,,,,, Pia watanzania naungana na Kubota Tunapaswa kumshukuru sana mchina kwa namna nyingi sana,kwani kulingana na umasikini/uwezo wetu kupitia china tunapata uwezo mfano zana za kilimo- trectors, viwanda vidogovidogo na hata vikubwa, kuhamisha tecnologia kupitia china ni rahisi sana kuliko popote pale, infrastructures n.k.
Mkuu CONSULT asante kwa mchango wako, naendelea kufuatilia sana mjadala huu. Wengi tunaelewa na kuzikubali Theory za umuhimu wa viwanda kwa uchumi wa nchi na hayo mataifa mengi sana duniani yaliyoendelea kwa kutumia viwanda. Mtazamo wangu hapa siyo wa Theory bali REALITY ya Tanzania yetu ilikotoka na ilipo hivi sasa. Tulikotoka nchi ilijipanga vizuri sana kiviwanda, vilijengwa viwanda vingi sana kuanzia zana za kilimo, mbolea, nguo, baiskeli, magari (Nyumbu) n.k safari ikaanza kwa nguvu, baadae viwanda vingi sana vikayeyuka!

Tujipange basi tuvisimamishe tena! Lakini anaekuja na hoja ya kukebehi kuhusu mrundikano wa Bidhaa za China kuwa ni uhujumu kwa maendeleo yetu na ajira ya vijana anapaswa aonyeshe bila chenga jinsi China wanavyoingilia sera na mipango ya serikali yetu kiasi kwamba tunashindwa kusimamisha viwanda hapa Tanzania. Aje mchumi hapa aonyeshe kama kunamchezo mchafu na jinsi Wazungu na Wachina unavyoucheza kiasi kwamba wazawa hawawezi kukopeshwa mitaji ya kusimamisha viwanda! Je ni China imezuia wawekezaji kuja kuanzisha viwanda Tanzania? Hayo mataifa ya mashariki yalikaribisha wawekezaji je Tanzania mchawi wetu ni China na wazungu kuzuia uwekezaji kama wa Malaysia na Singapore?Mtuonyeshe jinsi ambavyo Wachina hao wanavyowalewesha akili viongozi wetu wasiuone huo ukweli kuhusu kuimarisha viwanda!

Ninakubali kabisa viwanda ni muhimu sana lakini kwa hivi sasa tununue vitu, mashine na mitambo ya viwanda toka kwa walionavyo, China, kuwalaani hao inahitaji uthibitisho kuwa ni kweli wametufanyizia tusijenge vyetu. Viongozi wetu wengi ni wabinafsi na hawana uzalendo PERIOD! Tatizo ni sisi wenyewe!
 
Back
Top Bottom