MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Kwa mujibu wa kanuni zinazoendesha bodi ya Ligi, hizi ndizo sababu pekee zinazoweza kusababisha mchezo wa Ligi kuu kuahirishwa.
KANUNI YA 9
KUAHIRISHA MCHEZO
Mchezo unaweza kuahirishwa kutokana na sababu yoyote kati ya zifuatazo:-
(a) Endapo timu ina wachezaji watano au zaidi katika timu ya Taifa;
(b) Endapo timu inashiriki katika mashindano ya Kimataifa na ina muda usiozidi siku sita kufikia mchezo wa Kimataifa;
(c) Sababu yoyote ya dharura nzito na yenye msingi itakayokubaliwa na TFF
(d) Mchezo wowote ulioahirishwa utapangwa tena katika tarehe itakayoamuliwa na TFF isipokuwa kama ni dharura ya mvua au dharura yoyote nyingine basi mchezo huo utachezwa siku inayofuata iwapo ratiba inaruhusu
(e) Iwapo mchezo ulishaanza na kuvunjika kwa sababu ya mvua au dharura yoyote nyingine; magoli yaliyofungwa katika mchezo huo yataendelea kuwekwa katika idadi ya magoli yaliyofungwa na wachezaji binafsi lakini si katika idadi ya magoli ya timu. Kadhalika kadi walizoonyeshwa wachezaji katika mchezo ulioahirishwa au uliovunjika zitaendelea kuhesabika.
(f) Taarifa ya maombi ya kuahirisha mchezo ni lazima itolewe kwa maandishi si chini ya siku 14 kabla ya siku ya mchezo, isipokuwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa binadamu.
Katika kanuni hii, Sijaona kipengele kwamba mchezo unaweza kuahirishwa kwa sababu ya timu pinzani kunyimwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja husika.Tumeshuhudia michezo na figisu nyingi katika michezo ya CAF ikiwemo wachezaji kupuliziwa madawa katika vyumba vya kubadilishia, wachezaji kuvamiwa hotelini nk. Lakini haujawahi kusikia mchezo wa CAF umeahirishwa kwa sababu hizo, sanasana hatua huchukuliwa baada ya mchezo ila mchezo husika huachwa umalizike kwani kwa kusimamisha mchezo husika madhara ni makubwa zaidi.Je, nani atarejesha gharama za tiketi, malazi ya hoteli, wafanyabiashara mbalimbali waliowekeza kwa ajili ya mchezo tarehe husika?.Ni mara chache sana mchezo ukaahirishwa. Ninaamini pia sababu hizohizo ndizo zilipelekea mchezo kati ya Pamba na Simba kuruhusiwa kuchezwa licha ya kuwepo kasoro kadha wa kadha, Ndivyo hivyo mchezo wa JKT Queens ambapo bodi ya Ligi haikuamua kuhamisha mchezo huo tarehe nyingine bali ilitoa adhabu hapo hapo, na mchezo ulihesabiwa na JKT Queens waliadhibiwa vikali. Naamini sababu hizohizo ndizo zilizoiadhibu Biashara utd.
Kama mchezo unaweza kuahirishwa bila sababu ya msingi, na TPLB wakaona ni sawa, Itafika wakati timu ya ligi haitakuwa tayari kwa mchezo itatafuta sababu yoyote na Bodi itabariki kwa kusogeza tarehe mbele.
Hii inaondoa kabisa ile lengo la kanuni kwamba "Timu isipofika uwanjani, basi timu pinzani itapatiwa alama 3 na magoli 3. Sasa kanuni hii ina maana gani kama kuna uwezekano wa kukaa na kuyamaliza na mchezo ukapangwa wakati mwingine, Kanuni hii ina maana gani?
Bodi ya Ligi inapaswa kujitafakari sana. Ninyi ndiyo mnaotunga kanuni na nyie ndiyo wa kwanza kuvunja kanuni.