Bodi ya Ligi mjitafakari upangaji Ratiba za Mechi

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Ligi nyingi kubwa Duniani ziliisha karibu wiki tatu sasa sie bado labda hadi mwisho wa mwezi huu ndio inasemekana tutamaliza!

Hii ni shida, tuombe hili lisijirudie tena msimu mpya ujao, unakuta timu inacheza leo mechi inayofuata ni baada ya siku 10! Ukiangalia sababu ya maana hata huioni.

Akina Konate,ander herera wapo nchini kutalii wanatushangaa tunaendelea na ligi..wakati wao ndio hasa huko kwao covid ndio ilisumbua sana

Haya hapa kwetu leo tarehe 17 timu zetu zimebakiza mechi tatu tatu mechi nne nne..lakini hadi sasa ratiba kamili ya kueleweka hakuna!

Tuombe bodi ya ligi tuondoleeni usumbufu huu haya yasijirudie.
 
Ligi nyingi kubwa Duniani ziliisha karibu wiki tatu sasa sie bado labda hadi mwisho wa mwezi huu ndio inasemekana tutamaliza...
Sisi tuna mambo ya kingese sana kwenye mpira wetu hasa kupanga ratiba....jambo lakujirudia rudia tuu.

Hii kwanza inatokana na ujinga wa mara timu ya taifa ipewe muda wa kujiandaa, mara mtu mechi yake iarishwe kisa mechi za caf.

Tunalalamika vilabu vyetu havina hela but yet ligi letu linaenda kwa muda mrefu hivyo timu zinaingia gharama ambazo zinaepukika kwa mpangilio mzuri wa ratiba. Ligi zina timu 20 sie timu 16 lakini sie ndio tunachelewa kumaliza kwa sababu ya maamuzi ya kijinga.

Jambo lengine ni kwamba hii anaharibu wachezaji wetu...mchezaji anakuwa na mapumziko kibao. Sasa huyu ana shindana vipi na mchezaji ambaye anatwanga saturday, tuesday na saturday tena? Tunahitaji upangaji mzuri wa ratiba. Ona sasa caf walishatia tarehe za mechi za champions league. August 12 sie huku sii ajabu timu bado zitakuwa wapo katikati ya pre season.
 
Mkuu salam kwako. Hebu angalia kidogo hii ratiba ya Ligi ya Misri
Na kwa hawa wamisri unasemaje?
Ahsante
 
Unaungwa mkono na Mimi kwa 100%
 
Hili tatizo ni kila mwaka, ila watakuambia kuhusu tatizo la usafiri kwani kuna timu zinatumia mabasi 😂 eg. Namungo, watoke lindi mpaka geita.

Lakin pia naona uzembe kwenye upangaj wa mechi
 
mwezi wote wa 5 hakuna mechi iliyochezwa eti kwa sababu wachezaji wameitwa timu ya taifa wakati wachezaji wa sub wapo kibao tu,makipa wa sub ,mabeki, midfielders,washambuliaji wapo tu kibao hata hivo key players mbali na simba na yanga hizi timu ndogo walioitwa wachache sana bado mechi inaahirishwa,Simba ilicheza kimataifa bila viporo waliporudi bado wachezaji walicheza.

Je hao key players walioenda timu ya taifa wangepata injuries ligi ingesimama? Jibu ni hapana , sasa why ligi isimame kwa ajili ya taifa stars yenyewe ya kuunga unga.

Pia kuokoa mda timu zinapoenda mikoani hadi mikoa kwanini wasipange round ziishe huko huko kuokoa mda ,siyo timu inatoka Mtwara kwenda Mbeya kucheza na mbeya city baada ya game wamalizane na mbeya kwanza ndo waende dar, mfano unakuta Mtibwa anatoka moro kwenda kucheza na mbeya ,akimaliza anarudi Dar kucheza na KMC akimaliza anarudiswa tena mbeya ,huu ni upumbavu sana
 
Alafu hao hao tunasema vilabu vyetu havina hela wakati ligi tunairefusha.
Jana bwana julio kasema kimasikhara ila ndio ukweli haya mapumziko timu zinashindwa kugharamikia kambi hivyo wanawapa off wachezaji. Wakifika kitaa wachezaji wanafanya yao...wakirudi mwalimu anaanza kupambana upya.
 
Na mwaka huu ndiyo wamefanikiwa Sasa🤣🤣........hakuna Viporo kabisa.

Binafsi Kwa Tz ili ligi iwe bora timu ziwe 12 hapo tunaweza pata ushindani bora na ligi kuisha Kwa muda
 
Kwann ligi isianze mapema(mfano mwanzoni kabisa mwa agasti) ili iishe mapema? Utakuta ligi inaanza septemba mwishoni.
 
Na mwaka huu ndiyo wamefanikiwa Sasa🤣🤣........hakuna Viporo kabisa.

Binafsi Kwa Tz ili ligi iwe bora timu ziwe 12 hapo tunaweza pata ushindani bora na ligi kuisha Kwa muda
timu 12 ingekuwa poa sana,ligi ingekuwa kali mno ,tatizo ligi inaweza isha mapema wakati nchi zingine hata round ya kwanza bado
 
timu 12 ingekuwa poa sana,ligi ingekuwa kali mno ,tatizo ligi inaweza isha mapema wakati nchi zingine hata round ya kwanza bado
Inapangiliwa tu vizuri,kinapigwa weekend Kwa weekend......timu inasafiri comfortably kabisa
 
Hili tatizo ni kila mwaka, ila watakuambia kuhusu tatizo la usafiri kwani kuna timu zinatumia mabasi 😂 eg. Namungo, watoke lindi mpaka geita.

Lakin pia naona uzembe kwenye upangaj wa mechi
Miundombinu yetu bado sio rafiki kama ya huko duniani hivyo hiyo sababu ina mashiko.
 
Miundombinu yetu bado sio rafiki kama ya huko duniani hivyo hiyo sababu ina mashiko.
Mi nakerwa sana na baadhi ya timu kuchagua viwanja tofauti na viwanja vyao rasmi, na hasa wanapocheza na Simba au Yanga. Naona ni kuchoshana tu, na tamaa ya kupata pesa nyingi. Kama ni hivyo, basi vilabu viwe vinagawana mapato ya viingilio, bila kutofautisha mwenyeji, au mgeni.
 
timu 12 ingekuwa poa sana,ligi ingekuwa kali mno ,tatizo ligi inaweza isha mapema wakati nchi zingine hata round ya kwanza bado
Ligi ya Tunis mpaka sasa bado haijaisha na bado raundi tatu. Ligi ya Congo ndio bado kabisaaa. Ligi ya Morocco bado raundi tano, ligi ya Misri bado kabisa, ligi ya Nigeria bado,
 
Bodi ya ligi wamejaa vilaza, time imeenda mwanza, mbeya au Dar kuna timu za ligi kuu zaidi ya moja inacheza jumamosi had I jumamosi kwanza wanaingia gharama za guest , chakula na posho za wachezaji walitakiwa wakicheza jumamosi jumatano wanacheza tens.
Timu inaenda kucheza kanda ya ziwa inafanya safari zaidi ya Mara tatu badala ya kufanya safari Mara moja tu kuokoa gharama za usafiri, malazi na chakula.
 
Ligi ya Tunis mpaka sasa bado haijaisha na bado raundi tatu. Ligi ya Congo ndio bado kabisaaa. Ligi ya Morocco bado raundi tano, ligi ya Misri bado kabisa, ligi ya Nigeria bado,
Tunia ligi yao ipo kama ya belgium ,mizunguko ikiisha wale top six wanakipiga tena bingwa apatikane
 
Tunia ligi yao ipo kama ya belgium ,mizunguko ikiisha wale top six wanakipiga tena bingwa apatikane
Saivi si ndio ipo raundi ya mwisho hiyo bado game tatu tatu tu
 
Utasikian mechi imeahirishwa kwa sababu rais alikuwa na mambo mengi na alitaka ahudhurie au mechi imesogezwa mbele kwa kuwa ambulance INA rangi nyeusi sio nyeupe tulioizoea.
Upuuzi mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…