Bodi ya ligi mmetubeba Simba

Bodi ya ligi mmetubeba Simba

Roboti Wa Nape

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2023
Posts
1,174
Reaction score
2,876
Na declare interest. Mi Mwana msimbazi damu.

Tuendeleee

Tukiachana na Ushabiki pale hakuna Kanuni inayotubeba Simba ya kutofika uwanjani, hiyo kanuni hatuna ndio maana kwenye taarifa ya Klabu hakuna nukuu ya kifungu cha kugomea mechi ila kwenye Kanuni kuna kifungu cha adhabu ya timu ambayo inagomea mechi kutokana na makosa ya Kikanuni😀! Ukitaka kuamini muulize Mtu yoyote umetumia Kifungu gani kugomea mechi, hakipo.

Kanuni iliyotumika hapo inaitwa UTU UZIMA DAWA,hapa SIMBA anajua anachokifanya tena vizuri mno kete imesukumwa, sasa TFF na BODI rasmi wamewekwa mtegoni endapo mechi italazimika kusogezwa mbele YANGA watauliza ni kwa mujibu kwa kifungu kipi? Endapo Yanga atagoma kucheza mechi iliyosogezwa mbele utamhukumu kwa kifungu kipi? Hapo ndipo utata ulipo leo hii Wanangu.

Sasa kuna Watu wanakumbushia ile Yanga aliyogomea mechi ya 2021 ile Kikanuni huwezi kumwadhibu Yanga kwakuwa mabadiliko ya muda wa mchezo ama venue yana muda wake maalum kuwasilishwa kwa Klabu zinazohusika na mchezo, hivyo ila Kikanuni Yanga walikuwa sahihi walitimiza takwa la kufika kisha kuondoka baada ya muda sahihi wa kuwepo uwanjani, ila hii ya leo ngumu kwa Simba, TFF na Bodi, Yanga yupo pembeni anausoma mchezo.

Kesi ishakuwa ngumu hii, Shahidi analetwa Kituoni na escort ya Polisi, ishakuwa ngumu, SIMBA atawakumbusha kuwa mnakumbuka huyu aligomea mechi na tukakubali kurudiana? Ndio kete iliyosukumwa hapo, Simba ana historia ya Utii huku Yanga ana historia ya kufuata kanuni😀
1741434243941.jpg
 

Attachments

  • 1741434243941.jpg
    1741434243941.jpg
    71.8 KB · Views: 1
Ukishabikia sana simba na Yanga kichwani zinaanza kuyeyuka.
 
Kwahiyo dogo ume Copy andiko la Farhan huko Instagram umelileta hapa kama lako, hongera sana kwa women's day
 
Timu zingine zikatae uhuni unaofanywa na yanga wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa kisiasa

Quote
Screenshot_20250308-152526_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom