Bodi ya ligi ya NBC PL, na hili nalo mkalitizame

Hapo nikiangalia na hali yenu ilivyo kwa sasa kazi mnayo,lakini mwaweza okota alama kwenye game mbili ya polisi tz na ya kmc

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Inshu hapa ni kwamba, ni kwanini bodi ya ligi wanashindwa kupanga ratiba yao vyema mpaka upuuzi kama huu unajitokeza. Kuchelewa kwangu kuja jukwaani kulalamika hakuondoi ukwelli kua bodi ya ligi walipuyanga katika hili.
Sasa ulitakiwa kuja kuliongelea mapema soon tu ratiba ilipotolewa, kuliongelea sasa hivi ni kujisumbua tu ndugu yangu hakuna kitakachobadilika
 
We nae ni hovyo kabisa, umeangalia Ratiba ya kagera au Geita?, Mmezoea kupendelewa mnakaa na viporo 12!!. Isitoshe Simba wiki mbili ni timu iliyokaa bila kucheza mechi Zaid ya wiki 2 wakati huo ndio zingine zikicheza....., Ratiba ya timu kucheza baada ya 5 unakuja kulalamika hapa??.
Upuuzi, kwahiyo unataka Bodi ya ligi waipumzishi Simba au waitoe kwenye mzunguko wa ligi??. Jibu ni jepesi kwako huna kikosi kipana ndio maana unalialia na bado Ratiba ya Caf ndio itawamaliza maana utacheza kimataifa utarudi NBC baada ya siku 2 ucheze 😅.

Ngada fc
 
Sasa ulitakiwa kuja kuliongelea mapema soon tu ratiba ilipotolewa, kuliongelea sasa hivi ni kujisumbua tu ndugu yangu hakuna kitakachobadilika

Mkuu tangu bodi ya ligi ikabidhiwe usimamizi wa ligi kuu toka TFF, ligi hsijawahi kuisha bila ratiba kupangwa upya wakati msimu unaendelea. Ratiba hii lazima itabadilika tu ikuzingatiwa Simba na Yanga zimesonga mbele group stages za CAF. Hivyo kwa kua bodi ya ligi mda wanao, wakalitazame na hili.
 
Ratiba huwa haipangwi upya Ila tu kunakuwaga na kusogezwa mbele Kwa baadhi ya mechi ili kupisha baadhi ya mechi za kimataifa mkuu, ndo Sisi tunaita viporo
 
Ratiba huwa haipangwi upya Ila tu kunakuwaga na kusogezwa mbele Kwa baadhi ya mechi ili kupisha baadhi ya mechi za kimataifa mkuu, ndo Sisi tunaita viporo
Dah.. Kama ndo hivyo it's too late. Acha Mnyama akapambane tu.
 
Dah.. Kama ndo hivyo it's too late. Acha Mnyama akapambane tu.
Yah Ila Ligi yetu hasa management zake bado zina makandokando mengi Sana na hiyo ya ratiba ni moja wapo,

Imagine kamati tu ya masaa 72 huwa inashindwa kutoa hukumu Kwa muda stahiki unakuta mechi imechezwa Leo hukumu inatolewa wiki ijayo

Hukumu ya Chama na Ki ndo ya kipuuzi kabisa Ligi yetu ina mechi chache round 1 game 15 kumfungia mchezaji mechi 3 kisa tu hakufanya fairplay ni upuuzi kiwango cha juu mno yaani hukumu ya fairplay inakuwaje na adhabu sawa na mtu aliyepata redcard ya kucheza foul mbaya, tena straight redcard huwa ni mechi moja tu
 
We topolo mi hapa nazungumzia inakuaje timu inacheza ugenini mechi 7 mfululizo na si kila baada ya siku 5? Umemielewa we topolo?
Ratiba ya hizi timu zako Geita na Kagera ni kama ifuatavyo:-




We topolo nioneshe ni lini hizo timu zako zimecheza au zitacheza mechi 7 mfululizo?
 
Mkuu umeongea vyema sana. Natamani sana TFF na Bodi ya Ligi wangeona maoni yako.
 
Ivi unajua ulaya kwa mfano ligi ya England uwa wanacheza kila baada ya siku 3 yaani hawana mambo ya kumsogezea mtu muda sijui ana UEFA kama wanavyopendelewa simba na yanga, waafrica mnataka burudani ya soccer iwe adimu? Acha watu wafanye majukumu yao mbona wewe kila siku kazini, na players iyo ndo kazi yao, ulaya ndo maana player akifika miaka 36 amechoka kwa sababu ya majukumu sio uku mchezaji unataka apumzike sana ili iwaje
 
Ni kweli Mkuu. Bodi ya ligi walitakiwa walione hili mapema. Athari ya hili inaweza tokea katika group stages za CAFCL.
Ivi mnafuatilia soccer kweli au ushabiki tu, ivi ulaya uwa wanapumzika kwa muda gani yaani mechi kabla ya mechi nyingine , ni siku 3 tu yaani hawaangalii mtu ana UEFA iyo ni juu yake, mambo ya kuisogeza mechi kisa champions ligi ayo ni mambo ya kishamba na upendeleo kwa simba na yanga na haitakiwi kwenye soccer
 

Uko sahihi Mkuu. Vipi huko ulaya nako timu hua zinacheza mechi 7 mfululizo za ligi wakiwa ugenini?
 
Kweli muzeye.
 
Uko sahihi Mkuu. Vipi huko ulaya nako timu hua zinacheza mechi 7 mfululizo za ligi wakiwa ugenini?
Nimeiangalia hiyo ratiba vizuri kuna kitu kikubwa sana umeishindwa kukizungumzia. Hiyo michezo 7 ni ndani ya round mbili tofauti kwa nini umeiwasilisha kama vile ni round 1?

Ukweli ni kwamba hapo ktk michezo saba minne ni ukamilisho wa round ya kwanza mchezo wa kesho utachezwa hapa hapa Dar es Salaam. Hiyo mitatu inayosalia Simba ataenda viwanja vya ugenini kama alivyocheza michezo mitatu mfululizo nyumbani mwanzo wa ligi.

Michezo mitatu baada ya break ya wiki mbili ni michezo ya round ya pili baada ya kumalizika round ya kwanza. Hapo hakuna uhusiano wowote ule na round ya kwanza. Kosa ulilofanya umewasilisha ni kama vile Simba anacheza mechi saba ndani ya round moja, kitu ambacho si cha kweli.

Nimeona pia kuhusu mjadala wa Kagera Sugar hao wao ukiangalia juu juu ratiba ya unaweza kudhani ni kama wana michezo mitano nyumbani mfululizo ila ukweli hiyo ni michezo ndani ya round mbili tofauti. Watakamilisha mzunguko wa kwanza mechi mbili nyumbani baada ya break ya wiki mbili watacheza mechi tatu za mzunguko wa pili nyumbani.

Mapungufu pekee niliyoyaona juu ya hii ratiba kwa vilabu vyote, ni kwa nini waruhusu timu moja icheze michezo mitatu nyumbani au ugenini mfululizo ndani ya round moja? Nje hapa sijaona mapungufu yoyote yale makubwa juu ya hii ratiba kwa ujumla. Kuhusu michuano ya kimataifa kanuni za soka zinataka timu ipumzike masaa yasiopungua 48 baada ya mchezo mmoja yaani ni siku mbili kabla ya kupangiwa mchezo mwingine. Utaona ulaya timu inacheza alhamisi pia J'pili wanaingia uwanjani.
 

Mkuu nimekusoma vyema. Umeona kitu ambacho sikukiona. Japo ni raundi mbili tofauti kulikua hakuna haja ya Simba SC kucheza mechi 4 ugenini za kufungia msimu ugenini, alafu aje afungue ligi na mechi 3 za ugenini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…