Hamna kosa hapo Jombaa. Simba alicheza mechi tatu za kwanza nyumbani mfululizo sawa sawa na Kagera aliyecheza mechi tatu mfululizo ugenini za kwanza pia. Hiyo ni tradeoff tu ndani ya round moja.Mkuu nimekusoma vyema. Umeona kitu ambacho sikukiona. Japo ni raundi mbili tofauti kulikua hakuna haja ya Simba SC kucheza mechi 4 ugenini za kufungia msimu ugenini, alafu aje afungue ligi na mechi 3 za ugenini.
Round ya pili Simba atacheza mechi tatu mfululizo mara mbili nyumbani baada ya hizo tatu za mwanzo ugenini. Mapungufu makubwa ndani ya hii ratiba ninayoyaona ni kuruhusu michezo mitatu mfululizo timu moja icheze ugenini au nyumbani.
Pia kosa lingine la kiufundi kwa Simba na Yanga kuna michezo huwa ni kama wanaopanga ratiba huwa hawaihesabu ni kama ugeni kwa mf. michezo dhidi ya Ruvu na KMC.