Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungunza wakati wa zoezi hilo Afisa wa Maji Bonde la Wami Ruvu Kidakio cha Ngerengere, Mhandisi Nangu Makula amesema zoezi hilo litaenda umbali wa mita 900 kutoka Mazimbu hadi Kihonda.
Pia soma ~ Mto Ngerengere – Morogoro uchimbwe ili kuondoa taka zilizojaa, wakati wa mvua maji yanaingia mitaani
=============================
Wananchi wa Kata ya Mazimbu Darajani mkoani Morogoro wametakiwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kandokando ya Mto Ngerengere ili kuondoa changamoto ya maji kujaa katika mto huo. Maji hayo yametajwa kusababisha mafuriko kwenye makazi ya watu na barabara, na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kampasi ya Maharangu kushindwa kuvuka hivyo kukosa masomo.
Wito huo umetolewa na Afisa Kidakio cha Ngerengere Mhandisi Nangu Ngusa mkoani humo wakati wa zoezi la utiaji mchanga katika mto huo ambapo amesisitiza wananchi kuheshimu makatazo ya umbali wa mita 60 katika maeneo ya mito.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mazimbu Darajani Evod Kidea amesema kuwa wamekuwa wakipata changamoto ya maji kujaa katika makazi ya watu na kusababisha vifo hivyo kufukuliwa kwa mto huo kutakuwa na suluhu.
Pia soma ~ Wanaofanya uvuvi Mto Ngerengere eneo la Tungi na Kihonda wawe makini, kuna mashimo yaliyochimbwa wakati wa ujenzi wa SGR yana kina kirefu