Tanzania tuna import maziwa yenye thamani ya zaidi ya bil 500 kila mwaka ikiwamo maziwa ya azam yakitokea India na kuwa reconstituted.
Bodi ya maziwa walau ingejenga platform/bridge ili tuongeze capacity ya kuzalisha maziwa kama hao wauzaji wa ubungo na kuchakata pia.
Kwanini tunakosa innovators kwenye bodi za muhimu kama maziwa, kahawa, korosho. Labda niseme kitu, mara nyingi sana bodi huwa zinaongozwa na wastaafu au watu ambao wanakaribia umri wa kustaafu.
Ningeshauri kwa baadhi ya bodi maziwa na vijana wenye maono ya namna gani tunaweza ku-invent the wheel.
Bodi inge-open avenue ya kuwa na policy na kushirikiana na wizara ya mifugo na wizara ya fedha ili kuziba pengo la ku-import UHT milk kwa kuhakisha uzalishaji unafanyika ndani.
Watanzania wenye uwezo wa kuanzisha miradi kama hii tupo, fedha za uwekezaji mwaka jana zimebaki nyingi tu TIB kwa mujibu wa waziri wa fedha wakati anasoma bajeti. Wangeondoa urasimu kwenye access ya investment credit, nchi hii ingekuwa kwa haraka kiuwekezaji na kuwapa Watanzania unafuu wa bei ya maziwa badala ya kutegemea imports.
View attachment 1489881
Hii ni moja ya falsafa ya uongozi ambapo hata bodi ya maziwa wanawajibika kutafuta uhitaji wa watu/wadau kwenye sekta ya maziwa ili kuikuza sekta ya maziwa.