Kijana pole sana,naamini siku moja utakuwa na uwezo mkubwa wa kuang'amua mambo na utajilaumu kwa post hii.

1. Kuishukuru bodi ya mikopo inaonesha ulivyo na utegemezi wa mawazo. Ni jukumu la serikali kuhakikisha unapata mkopo hivyo kupata kwakwo na wengine kukosa usione kama bahati, ni haki yako. Na wengine wana haki na wajibu wa kudai mpaka wapate haki hiyo

2. Kusema vigezo vilivyotumika vimewaokoa wanyonge si kweli, bahati mbaya unaoweza kuwaita wanyonge wezio wamekosa. Rejea taarifa ya Bodi (waliokidhi vigezo ila hakuna fedha).

3. Kwamba watoto wa matajiri wanasoma shule nzuri ni kweli. Kwamba wanaiba mitihani na kupata one ni dhana potofu. Huna ushahidi kuthibitisha hoja yako na naamini huenda uliwahi kusikia "eti..." na si kwamba ulishuhudia. Si vyema kudharau mafanikio ya wenzako

4. Kwamba wakifika vyuoni wanatanua tu, si kweli. Kwanza umejauaje? maana hujawahi kusoma huko na kama uliambiwa huenda ulipewa taarifa potofu. Chuo kikuu sio sehemu ya mtu kutanua tu, tena kwa mtu asiye na uwezo darasani. Kama wanatanua na wanafaulu basi hao sio viraza kama unavyo wafikilia. Katika lugha nyingine hizo one ni za uhakika.

Mdogo wangu jaribu kuachana na mawazo ya umimi. mawazo ya kwa vile nimepata wengine watajiju. Dunia haiendi hivyo, serikali inaweza kubadili sera na ikakuumiza ukiwa hata hujamaliza mwaka wa kwanza wa masomo (kumbuka iliwahi kutokea). Pia unaweza kudisco ukalazimika kuomba upya mkopo, yakakukuta.

Be careful with what you say especially in this period where thousands of sons and daughters of this country have lost hope and don't know what their destiny will be. Tunahitaji kuwatia moyo na si kuwadhihaki