Bodi ya mikopo mwaka huu 2012/2013=msiba

Bodi itatoa mkopo kwa zile kozi wanazohitaji na nazan kabla kutaka kuomba mkopo bodi ilishauri mtu aangalie priority na non priority. Na kuhusu swali na kuzaa ni bora mtu apange uzazi wake kulingana na kipato chake na si kutegemea kila mtoto ana riski yake. But kwa upande mwengine wapo pia wazazi waliopata mtoto mmoja tu na bado wanashindwa kumsomesha elimu ya juu na hii ni kutokana na system mbovu ya uchumi ya nchi yetu ambao hauwezi kumsaidia mwananch wa kawaida licha ya kauli mbiu ya Taifa ya maisha bora kwa kila Mtanzania
 

mkuu,kuna EGM wamepata enginearing&archtecture na zina loan priority,kuna HGE&HGL&HGK wamepata LMV na ina priority,agrbuznec ya sua the same
na pili tutambue maana ya neno non priority na priority kwanza,hazimainishi hukuna mkopo bt hakuna kipaumbele ktk utoaji wa mikopo
 
Wa2 wanachanganya mambo kama una div1 kwa mvulana na div1&2 kwa msichana unapata mkopo bila wacwac ila km una matokeo chini ya hapo na umedahiliwa hapo ndipo suala la vipaumbele huangaliwa maana yake hata kma una div3 but umekuwa admitted kwenye hizo course zenye priority utapata mkopo kwa viwango walivyoanisha suala la priority litakuja km huna matokeo niliyotaja hapo juu huo ndio ufafanuzi niliopata toka ofisi za bodi
 
Kaka criteria za mwaka gan huo?!na umeconfirm kwa nan bod?!!
 

Nikurekebishe kidogo kwenye koz za education upande wa arts bodi inasema watapata mkopo "of not less than 50%" maana yake usiopungua asilimia hamsini, Sasa wewe unasema "of not more than 50%" usiozid asilimia hamsini. Hakuna kitu kama hicho hebu kasome vizuri Guidelines and criteria.
 

kaka mkopo hauna relation na matokeo yako,dv 1 or 2 cyo gurantee ya mkopo,kama umesoma vzr hicho kipengele kilishafutwa kitambo baada ya kupigiwa kelele bungeni.
 
Majuta tcu na ccm na tcu wanata watu wacende vyuo ili kukwepa lawama za ajira na wajiunge na kilmo kwanza
 

uko sahihi sana mkubwa,, that is the way it supose 2 be!
 
mi naona 2ngepewa 2 angalau 0% ya accomodation then ada 2jilipie wenyewe maana ada ni ya kawaida haina shida! Shida ipo kwenye ela ya ku2mia!
Angalau wange equalize wa2 wote wapate zero then wajilipie wenyewe ada kuliko kuwapa wa2 100%, 90% wakati wengine no loan at all! Hii ingeleta usawa na kuondoa mambo ya usayansi¡,
cku hzi wa2 wanasoma kuangalia mkopo na cyo kile wanachokiweza!
Heslb inabdi kuangalia hlo, maana mkopo ni kwa ajili ya watanzania waciojiweza na cyo kwa wanafunzi wa sayansi!
 

true, kwa kufeli kuelewa criteria barabara hata ufaulu wake una mashaka.
 
Hivi huyu mdau aliyeleta hoja hii ya wanafunzi kukosa mikopo kaitoa wapi? anafanya kazi HESLB? Taarifa yake inaonekana ni ya mtaani. Sisi tumefuatilia hadi sasa Bodi haijatoa majina ya wale wanaopata mikopo na hata mwongozo ule wa mikopo haujasema chochote kuhusu suala hilo. Tusiwekane roho juu jama!
 
Nafikiri si sawa kuomba course kwa sababu tu mtu atapata mkopo, hebu kila mtu asome kitu anachoona ndo kitamfikisha kwenye ndoto zake--
 
Nafikiri si sawa kuomba course kwa sababu tu mtu atapata mkopo, hebu kila mtu asome kitu anachoona ndo kitamfikisha kwenye ndoto zake--

Unachokisema ni kweli,lakini kumbuka tatizo ni Pesa. Hakika mimi mwenyewe kama sio wafadhili wa nje na ndani walinisaidia,pengine hata elimu ya form 4 nisingeipata kama alivyoikosa dada yangu. Siwezi kulaumu sana,lakini hali ya wazazi ndivyo ilivyo. Nilihitimu form 6 mwaka jana,ilinilazimu kukaa mtaani mwaka mzima kwa kukosa mkopo baada ya kuchaguliwa program ya biashara ambayo ndiyo lilikuwa tamanio langu. Mwaka huu imenilazimu kuomba education ili nipate loan,nikiona vipi baadae ntabadili.
 

kaka umetumia kigezo gani kupima uwezo wa kila mtanzania aliyeomba hii mikopo? Naamini hukushirikisha ubongo wako vyema. Kwa taarifa yako ni kwamba,mimi binafsi kama sio misaada niliyoipata,hata elimu ya form 4 nisingeipata. Sasa leo unashauri kwamba tupewe tu ela ya matumizi,na hii ada ya mil 1.6 mtu kama mimi ntaipata wapi? Na sio mimi pekee,naamini kuna watanzania wengine kama mimi. Naomba ukae tena chini,na uandike mambo yenye tija katika jamii,na sio kuangalia tu uwezo binafsi.
 
Kaka nakubaliana na wewe lakini najaribu kuona namna kesho yetu itakavyokuwa na watu wenye elimu kubwa kwa fani wasizozipenda na wala hawana wito nazo, mfano wewe na biashara kama fani yako pendwa uende kupigisha watoto shule lazima elimu yetu ishuke sababu najua ni lazima utatamani hiyo shule uieguze biashara ili utimize ndoto zako--
 

hapo sina cha kusema,ila haya mambo yameshakuwa usanii mtupu. Ila kwa upande wangu,kama nikiwa mwalimu,ntaifanya kazi yangu kwa uaminifu. Nikiona nimeingia choo cha kike,ntabadili fani. Unayoyasema ni kweli kabisa.
 
mkuu kama unavyoelewa hali halisi ya tz kwa sasa!! ni ngum sana kuwafinance watu wote...na wanachotaka sasa ni kuchek zile areas ambazo hatuna wataalam wa kutosha mf engineers,wanakilimo,teachers, na madokta!!! sio kwamba wanapenda iwe hivyo ila ndo hali halisi...serikali imefulia...
 
well said!!!
 
Hamna cha kufulia serikali inao uwezo mkubwa tu wakuwasomesha raia wake,pesa ngapi zinaliwa na mafisadi mabilion kwa matrilion izo pesa zingesomesha watoto wangapi? Tatzo watanzania tunakubaliana na kila kitu bila kuhoji kuna taarifa kuwa viongozi wa bodi ya mikopo wanalipwa hadi milion 12..kwa kazi gani hasa,inauma sana ukitaka kufatilia vitu kwa undani pexa zenyewe ni hizi za baba walipa kodi kati kuna wafanyabiashara wakubwa na vigogo wanakwepa kulipa kodi..ndia maana watanzania wengne wakpata nafasi ya kwenda nchi za nje hawataki hata kurudi nchini mwao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…