Bodi ya Mikopo: Tumepokea maoni kuhusu changamoto ya mfumo kwa waombaji wa Diploma, tunashughulikia changamoto hiyo

Bodi ya Mikopo: Tumepokea maoni kuhusu changamoto ya mfumo kwa waombaji wa Diploma, tunashughulikia changamoto hiyo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kulalamikia changamoto ya mfumo wa HESLB kwa waombaji wa Stashahada (Diploma) wanaotarajiwa kudahiliwa Machi 2025 (March Intake), ufafanuzi umetolewa na mamlaka husika.

Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ Mfumo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu umekuwa na changamoto wiki hii, haupokei maombi ya wahitaji kwa siku ya 9 leo

UFAFANUZI WA HESLB
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imepokea changamoto wanayopata Wanafunzi wa Stashahada wakati wa uombaji mikopo hususan katika eneo la kuingiza taarifa za RITA.

Kwa wale mnaokumbana na changamoto hii, tumepokea na tunaishughulikiwa ili kila mwombaji wa mkopo wa Stashahada mwenye sifa aweze kuwasilisha maombi yake kwa kuweka taarifa zake kwa usahihi.

Aidha, mpaka sasa kuna maombi 1,713 ya Stashahada ambayo yako katika hatua mbalimbali za uhakiki.

Tunawahakikishia waombaji wote wanaoendelea na zoezi la uombaji mikopo kwamba kwa kuzingatia changamoto mbalimbali ambazo baadhi yake zipo nje ya uwezo wetu watapata muda wa kukamilisha zoezi hilo.
 
Sikuhizi watoto wengi wanakwepa Advance labda maombi ya diploma ni mengi mpaka yanawazidia.
 
Back
Top Bottom