copyright
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 584
- 584
Salaam!
Ni jumanne iliyo njema sana.
Moja Kwa moja kwenye mada.
Bodi ya Mikopo (HESLB) imekuwa ikiwaangamiza watumishi wa umma ambao waliwahi kuwa wanufaika wao walipoamua kujiendeleza kielimu bila kuzingatia kanuni ya 1/3 (Moja ya Tatu) ya mshahara. Nimeshuhudia na/kuona watumishi wakipokea TSH 110000/= (Laki moja na Elfu Kumi tu) kama mshahara wa mwezi mzima.
Na Kwa namna nyingne wamekuwa wakiwakata watu ambao hawakuwahi kuwa wanufaika wa Mikopo yao na kusababisha usumbufu usio na sababu kwa watumishi hao, kwani hulazimika kwenda makao makuu ya HESLB kwa nauli na gharama zao pasipo kurudishiwa au kupewa pesa za usumbufu.
Hali hii haikubaliki na sio nzuri kwani inashusha ali katika kufanya kazi, inachochea sana watu kuchukia kazi zao, inaongeza ugumu wa maisha kwa watumishi wa umma na familia zao.
Ni wakati sasa Prof. Mkenda kufuatilia suala hili ili kusaidia maisha ya watumishi hawa wa umma pia Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo (HESLB) kutafuta mbinu nzuri ya kukata watumishi bila kuathiri moja ya tatu ya mshahara.
Mungu Ibariki Tanzania.