KERO Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) inaangamiza watumishi wa umma

KERO Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) inaangamiza watumishi wa umma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Salaam!
Ni jumanne iliyo njema sana.

Moja Kwa moja kwenye mada.
Bodi ya Mikopo (HESLB) imekuwa ikiwaangamiza watumishi wa umma ambao waliwahi kuwa wanufaika wao walipoamua kujiendeleza kielimu bila kuzingatia kanuni ya 1/3 (Moja ya Tatu) ya mshahara. Nimeshuhudia na/kuona watumishi wakipokea TSH 110000/= (Laki moja na Elfu Kumi tu) kama mshahara wa mwezi mzima.

Na Kwa namna nyingne wamekuwa wakiwakata watu ambao hawakuwahi kuwa wanufaika wa Mikopo yao na kusababisha usumbufu usio na sababu kwa watumishi hao, kwani hulazimika kwenda makao makuu ya HESLB kwa nauli na gharama zao pasipo kurudishiwa au kupewa pesa za usumbufu.

Hali hii haikubaliki na sio nzuri kwani inashusha ali katika kufanya kazi, inachochea sana watu kuchukia kazi zao, inaongeza ugumu wa maisha kwa watumishi wa umma na familia zao.

Ni wakati sasa Prof. Mkenda kufuatilia suala hili ili kusaidia maisha ya watumishi hawa wa umma pia Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo (HESLB) kutafuta mbinu nzuri ya kukata watumishi bila kuathiri moja ya tatu ya mshahara.

Mungu Ibariki Tanzania.
kwa bahati mbaya, wengi walivumilia hadi mkopo ukalipwa wote. dawa ya deni ni kulipa, hakuna namna ndugu.
 
Sure, na me nimeshuhudia watumishi watatu tofauti walioko masomoni wakipokea Tshs. 131,000 kwa mwezi baada ya kuanza kukatwa na HESLB Kabla hata ya kumaliza masomo. Nashauri wangewaacha wamalize masomo kwanza ndo waanze kuwakata
Yeah yani ni mateso na ni kuumizana
 
Mfano mimi sikuwahi kupata mkopo nilisoma kwa kwa msaada wa wizara ya fedha (mof) nikashangaa nakatwa niliwafuata huko nikazingua mbaya wakarudisha kibunda.
Duh
Pole sana Mkuu lakini walirudisha zote
 
Lipeni medeni hayo na wenzenu wasome sio mnalialia hapa
 
Hivi kama mnufaika wa mkopo kutoka HESLB baada ya masomo ukaamua kujiajiri au ukafariki kuna namna Bodi inaweza kuwafanya wanufaika kulipa deni? Na je kwa upande wa waislam maana maiti kabla ya kuzikwa utaulizwa umma kama kuna mtu anamdai marehem je, kuna mikakati yeyote kufanya familia ya marehemu kulipa deni kwa dini zote?
Bila shaka hapana, mifumo yao ilivyosetiwa ni watakata direct kwenye mishahara na Kwa waliojiajiri wanapewa namna ya kudeposit marejesho yao
 
Ni wahanga pekee ndiyo wanayo yaelewa maumivu yake. Imagine hayo makato yao 15 jakija huwa hayaangalii umebakiwa na kiasi gani kwenye salary slip.

Kwa kweli kama mtu unajimudu, ni bora ukajigharamia mwenyewe/ukawagharamia watoto wako masomo ya chuo kikuu, ili kujiepusha/kuwaepusha na madhara yatokanayo na hiyo Bodi.
Kabisa kabisa mkuu
 
Kinachonishangaza sana ni hili;

Bodi hukuti imesahau kusitisha mkopo baada ya kutambua umekwisha hitimu ila itasahau kusitisha makato baada ya mwajiri kukamilisha deni lake. Ndo hapo unakuta unaenda makao makuu kila mwezi kuwakumbusha kuwa deni lao mbona wamekwisha mapiza. Ogopa hiyo
Wana makando kando mengi sana af yanatuumiza sisi
 
Sheria hairuhusu shida hawawez jua huyu ni mtumishi au sio mtumishi.me jamaa zangu 2019 walipata asilimia 100% wengi tu tena waajiriwa.
Uwezo wa kujua wanao ila hawajaamua bcoz waajiriwa ndo wenye uhakika wa kulipa so ni ngumu kuwaacha na kuchukua freshers tupu
 
Back
Top Bottom