conoralbert
New Member
- Jul 29, 2023
- 3
- 1
Katika hali ya kushangaza mfululizo wa hali ya ucheleweshwaji wa malipo ya pesa ya kujikimu na chakula kwa wanafunzi wa vyuo Vikuu imekuwa ni jambo la kawaida sana kufanywa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu HESLB. Tunaomba kila mwenye ushawishi asaidie kupaza sauti juu ya hili.
Updates...
UCHELEWESHAJI WA MIKOPO YA PESA ZA KUJIKIMU (BOOM) AWAMU YA NNE KWA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM ( UDSM).
Mimi ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kampasi Kuu ya Mwalimu Nyerere.
Kwasasa kuna changamoto ambayo wanafunzi wengi tunaipitia ni ucheleweshwaji wa pesa za kujikimu (meals and accomodations) maarufu kama BOOM.
Kwa kawaida pesa hii huingia baada ya wiki nne za masomo au siku 60 ambapo ni sawa na Miezi 2 kwa semester na kwa mara ya mwisho pesa hii iliingia tarehe 22/03/2025 lakini cha kushangaza mpaka wakati huu naandika haya pesa hii haijaingia ikiwa ni tarehe 28/05/2025, waliongiziwa ni wanafunzi wachache sana hapa chuoni.
Kitu kinachotushangaza na kutusikitisha ni kwamba hakuna taarifa yeyote kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB) kuhusiana na ucheleweshwaji huu wa pesa ya kujikimu.
Kimsingi hali za wanafunzi ni mbaya sana, uendeshaji wa maisha umekuwa mgumu, tunaziomba mamlaka husika yaani wizara ya Elimu na Bodi ya mikopo kutoa ufafanuzi na kuingilia kati suala hili kwani wanafunzi wengi wanateseka na ugumu wa maisha kwa kukosa stahiki zao kwa wakati kwani Boom ndilo linawezesha wanafunzi kujikimu wanapokuwa chuoni.
Naomba kuwasilisha, Asante.
Majibu ya HESLB, soma hapa ~ Bodi ya Mikopo yasema changamoto ya mifumo ya Kibenki imechangia 'Boom' kwa Wanavyuo kuchelewa