The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mnamo tarehe 28 Septemba bodi ya mikopo HESLB ilianza kutangaza waliopangiwa mkopo awamu ya kwanza yenye wanafunzi 21,509 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/2025.
Kadhalika Bodi ya Mikopo ya Wanafurnzi wa Elimu ya Juu (HESLB) siku ya Jumatano (Oktoba 09, 2024) ilitangaza awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2024/2025.
Kilichonishangaza ni baada ya kutembelea Chuo kimoja kilichopo jijini Dar es salaam na kukutana na mtu ambaye ni mtumishi hapo na kunieleza kuwa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) wamefuta allocations walizokuwa wamezitoa kwa wanafunzi ambao walikidhi vigezo huku sababu ya kufuta allocations hizo ikiwa haijulikani na kuwaacha njiapanda baadhi ya wanafunzi wanaotegemea mikopo hiyo huku vyuo vikiwa vimeanza kufunguliwa.
Swala hilo likanifanya nitafute mwanafunzi ambaye alipangiwa mkopo ili kuthibitisha hilo na baada ya kuangalia account aliyotumia kuomba mkopo hivi ndivyo inavyoonekana.
Awali kabla ya hilo kutokea allocation yake ilikuwa ikionekana hivi
Mpaka sasa bodi ya mikopo hawajasema chochote juu ya jambo hili wakati ambao baadhi ya vyuo vikiwa vimefungua na usajili wa wanafunzi ukiendelea HESLB ni vema mkatoa ufafanuzi haraka sana.