Bodi ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu wamefuta allocations za wanafunzi ambao walipangiwa mikopo 2024/25

Bodi ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu wamefuta allocations za wanafunzi ambao walipangiwa mikopo 2024/25

Kuna mwingine kaandikiwa hivi inasikitisha sana
 

Attachments

  • Screenshot_20241013_234200_Chrome.jpg
    Screenshot_20241013_234200_Chrome.jpg
    136.7 KB · Views: 9
Mwanangu mwaka juzi alipata mkopo Bach one. Nikascreen shoot kabisa maandalizi yakafanyika akafika chuo.
Tobaaaa kuja kwenye harakati za usajiri system ya chuo inamkataa aimtambui kama mnufaika wa mkopo.
Kuja kuchungulia sipa yake Sasa mkopo Amna umefutwa tumekalibishwa dilisha la rufani nikasema ujinga huo sifanyi akuna rufani hapa.
Nb.bodi ndio tabia yao kiwanusishwa mikopo watoto wa watu then wanawakwapua juu kwa juu.
Hii ni changamoto hasa kwa wanafunzi wanaotegemea mikopo hiyo kulipa ada
 
Daah pole sana kwa wanufaika, alafu ukute anasomea corse ya Management of social development hapo bora uende ukasomee ujuzi veta kuliko kuhangaika mwisho wa siku unaanza kukatiza mitaa ya posta na bahasha ya khaki.
 
Mnamo tarehe 28 Septemba bodi ya mikopo HESLB ilianza kutangaza waliopangiwa mkopo awamu ya kwanza yenye wanafunzi 21,509 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Kadhalika Bodi ya Mikopo ya Wanafurnzi wa Elimu ya Juu (HESLB) siku ya Jumatano (Oktoba 09, 2024) ilitangaza awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2024/2025.

Kilichonishangaza ni baada ya kutembelea Chuo kimoja kilichopo jijini Dar es salaam na kukutana na mtu ambaye ni mtumishi hapo na kunieleza kuwa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) wamefuta allocations walizokuwa wamezitoa kwa wanafunzi ambao walikidhi vigezo huku sababu ya kufuta allocations hizo ikiwa haijulikani na kuwaacha njiapanda baadhi ya wanafunzi wanaotegemea mikopo hiyo huku vyuo vikiwa vimeanza kufunguliwa.

Swala hilo likanifanya nitafute mwanafunzi ambaye alipangiwa mkopo ili kuthibitisha hilo na baada ya kuangalia account aliyotumia kuomba mkopo hivi ndivyo inavyoonekana.


Awali kabla ya hilo kutokea allocation yake ilikuwa ikionekana hivi


Mpaka sasa bodi ya mikopo hawajasema chochote juu ya jambo hili wakati ambao baadhi ya vyuo vikiwa vimefungua na usajili wa wanafunzi ukiendelea HESLB ni vema mkatoa ufafanuzi haraka sana.
wawe na subira tulipo tuna kikao kifupi tumebaini hela tuliyowapa ilikuwa kimakosa nawengine wamecomfirm chuo zaidi ya kimoja,yaani leo anakomfirm chuo x baada ya siku tatu an uncomfirm kisha ana comfirm chuo y. na pia tanampango wa kuwapunguzia kiasi ili na wengine wote wapate kidogokidogo
 
Ukiachana na allocation
kuna vyuo pia wanafunzi wanakuta kwenye account zao kua admission rejected
uhuni sana nimeingia mzumbe kwa mdogo wangu eti wananiambia comfirm nikijaribu mfumo unaniambia nafasi imeshajaa kwa kozi hiyo, wakati kabla nilisha comform na admission letter nime-print pamoja na joining instuct
 
Waheshimiwa mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa chuo cha tumaini dar es salaam ( TUDARCO) niliomba mkopo sijapata na nasoma course ya sheria na mpaka saivi nafikiria kuhairisha masomo kutokana na ugumu wa maisha nilikuwa naomba unisaidie japo ada tu ya chuo au nisaidie mawazo niweze kujua na nilipata division one
 
Waheshimiwa mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa chuo cha tumaini dar es salaam ( TUDARCO) niliomba mkopo sijapata na nasoma course ya sheria na mpaka saivi nafikiria kuhairisha masomo kutokana na ugumu wa maisha nilikuwa naomba unisaidie japo ada tu ya chuo au nisaidie mawazo niweze kujua na nilipata division one
Issue Yako very sensitive anzishia thread mpya kabisa utapata wadau wa kukusaidia.
Pole Kwa changamoto issue unayopitia nami nilipitia miaka kadhaa nyuma lakini mungu ni mwema wadau walinishika mkono na chuo kiliisha salama kabisa
 
Back
Top Bottom