Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Tsh. Milioni 623.2 zatumika kuwafadhili
■Jumla ya wanafunzi 80 wa Shahada za Uzamili katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) ambao wamedahiliwa katika programu za sayansi na ubunifu, wamepangiwa ruzuku zenye thamani ya TZS 623.2 milioni kupitia 'Samia Scholarship'.
■Wanafunzi walioomba fursa hizo wanashauriwa kuangalia taarifa zao kupitia akaunti walizoombea (SIPA). Aidha, wanafunzi husika watatakiwa kujisajili kwenye mfumo wa malipo wa kidigitali (DiDiS) kupitia kwa Maafisa wa HESLB watakaoratibu zoezi hilo chuoni NM-AIST kuanzia Januari 22, 2025.
■Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoa 'Samia Scholarship' kwa wanafunzi wa fani za Sayansi waliodahiliwa katika ngazi ya Shahada za Uzamili.
■Kwa taarifa hii, wanafunzi wote walioomba fursa za 'Samia Scholarship' katika ngazi ya Shahada za Umahiri wanajulishwa kuwa zoezi la upangaji ruzuku hizo kwa mwaka 2024/2025 limefikia mwisho.
Imetolewa na: Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Dar es Salaam, Januari 22, 2025
Pia soma ~ Wanufaika wa Ufadhili wa Masomo ya Masters kupitia Samia Suluhu Scholarship tumetelekezwa bila muongozo