Bodi ya Nyama Tanzania yapiga marufuku uuzaji wa nyama za mafungu

Bodi ya Nyama Tanzania yapiga marufuku uuzaji wa nyama za mafungu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Bodi ya Nyama Tanzania imepiga marufuku uuzaji wa nyama kwa mafungu katika maeneo ya nje ya machinjio ya vingunguti kwani inahatarisha afya ya mlaji.
.
Hayo yamesemwa na Kaimu Msajili wa bodi ya Nyama Tanzania Bw. Imani Sichalwe alipofanya ziara katika maeneo ya nje ya machinjio ya vingunguti na kusema uuzaji wa nyama kwa mafungu kiholela haukubaliki kwa mujibu wa Sheria na unaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa Kama kipindupindu na magonjwa Mengine ya matumbo kwa kuwa maeneo hayo ni machafu kuna mifereji ya maji taka kutoka katika vyoo na ni Maeneo ya wazi ambapo Kuna vumbi na kuhatarisha usalama wa nyama.

nyama%20za%20mafungu%202.jpg

Bw.Imani Sichalwe amewataka wauzaji wa Nyama hizo kwenda katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya biashara hiyo lakini sio Maeneo Kama yale ya wazi.
.
"Hapa tunaona kinyesi na mikojo karibu na mnapouzia Nyama kwani ninyi hamuoni Kama ni hatari kwa afya,mlipuko kwa magonjwa ukitokea wa kwanza ni ninyi ambao hamfuati utaratibu hapa."Amesema Sichalwe.
.
Hata hivyo amesema kuwa dhumuni la serikali sio kuwakataza watu kufanya biashara bali kuwashawishi wafanyabiashara kufanya biashara zao katika hali nzuri na kuzingatia afya kwa mlaji.
 
Huku kwetu nyama ya mafungu ndio maisha unapata kuanzia mapande ya nyama ya ng'ombe, mbuzi, samaki, kuku hadi utumbo wao, pamoja na miguu na vichwa vya kuku😛😛😛 tena bei rahisiiii hadi mia5 unakula.

Bodi wajipange tuu jinsi ya kuwapa wauzaji miongozo kuboresha usafi.
 
IMG-20210314-WA0016.jpg
 
jamaa kaongea kwa hisia sana,sasa mtu unamfanyia hayo kupambana na wewe hawezi kwa nini asikuombee dua ufe??na mkifa lazima watu washerekee vifo vyenu kwa sababu ya dhulma
 
Kama shida ni mikojo na uchafu?
Basi dawa ni kuondoa mikojo na huo uchafu!
Ili Huduma ziendelee!
HAPA KAZI [emoji123][emoji106]
 
Huku kwetu nyama ya mafungu ndio maisha unapata kuanzia mapande ya nyama ya ng'ombe, mbuzi, samaki, kuku hadi utumbo wao, pamoja na miguu na vichwa vya kuku[emoji14][emoji14][emoji14] tena bei rahisiiii hadi mia5 unakula.

Bodi wajipange tuu jinsi ya kuwapa wauzaji miongozo kuboresha usafi.
Ndy muache nunua nyama za mafungu
Sasa mshapigwa marufuku

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom