Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Mjumbe wa Bodi ya Simba SC CPA ISSA MASOUD akiongea na Waandishi wa habari Jana, amekiri kwamba shilingi bil. 20 alizoahidi mwekezaji Mohamed Dewij "Mo" hazijawahi kuwekwa popote Bali aligeuza fedha anazotoa Kwa matumizi ya kawaida (kununua mchicha, boxer na kandambili) ndo zihesabike kama uwekezaji wa 20b.
Alichotushangaza zaidi ni pale aliposema Jambo hili wanalijua Kwa miaka 3 Sasa lakini wamekuwa wakitoa Taarifa ya Bodi kwenye mikutano mikuu kuonyesha Mambo ni shwari.
Akaenda mbali zaidi akasema hata usajili wa Wachezaji unafanyika Kwa kificho Bodi haijui na kwamba kuanzia Sasa hawataruhusu hilo maana Hali hiyo imesababisha kusajiliwa Kwa Wachezaji wasio na kiwango Bora cha kuchezea Simba SC.
Hoja yangu ni kwamba, Kwa nini Bodi hii hasa wajumbe waliochaguliwa na wanachama wamekubali Kwa miaka yote 3 kuwauza wanachama waliowachagua na kuungana na wajumbe wa upande wa Mwekezaji kutengeneza Taarifa feki na kuwasomea wanachama kwenye mikutano mikuu?
Kwa hali hii nini faida ya wanachama kuwa na wawakilishi kwenye Bodi kama nao wanaungana na mwekezaji "kudanganya" wanachama? Hata kama lengo ilikuwa kutunza Siri za Bodi, walitegemea kutunza Siri hii Kwa Muda gani?
Kwa hili wajumbe wa Bodi mliochaguliwa na wanachama mmewauza waajiri wenu, Wajibikeni.
PIA SOMA
- Wajumbe Bodi ya Simba upande wa Wanachama wagoma kujiuzulu
- Salim Abdallah 'Try Again' ajiuzulu uenyekiti bodi ya wakurugenzi Simba
- Bodi ya Simba upande wa mashabiki wanataka kumtapeli Mo Simba yake
- Tetesi: - Simba imepasuka. Kuna Simba ya Try Again na Simba ya Mo, Kila upande unauroga upande mwingine
- Tetesi: - Simba inatarajia kumrejesha tena Barbara Gonzalez kwenye Bodi