Bodi ya Simba SC mmekiri mmewauza wanachama kwa miaka 3, wajibikeni

Kipindi simba inafanya vizuri hali ilikuwa shwari leo hii MO amekuwa mtu mbaya kweli shukran ya punda mateke.
 
Katika maisha yangu, anayepinga jambo Huwa nampa attantion zaidi kuliko anayesifia. Kigwangala nilikuwa namuelewa Sana anachokilalamikia ila tu Kwa sababu Mo alikuwa ashawarubuni wajumbe na uzuri akachukua ubingwa waliomlalamikia wakaonekana wananongwa tu.
 
Haya tuchukulie kuwa MO ana matatizo ya ujanja au hata utapeli halafu kuna mjumbe wa bodi aliyeaminiwa na wanachama ambaye ni CPA (T) halafu yupo anaona madudu yote hayo ya Mo akaamua kukaa kimya kwa miaka 3+. Ghafla tu leo anaibuka kwenye vyombo vya habari bila aibu anasema kwa takribani miaka mitatu kuna matatizo Simba!

Swedi Mkwabi apewe maua yake kwa sababu yeye aliona madudu mapema na akajiuzulu lakini hao wapuuzi wakina CPA Masoud hawana cha kujitetea kwani wao ni sehemu ya hayo madudu yote wanayomuangushia Mo sasa hivi.
 
Hatari sana.
 
 
Kwangu mm naona wanapata hela zisizo na jasho plus strip zinazogharimiwa na account ya simba ndio maana hata sasa hawapo baada ya kuchuma hela ya kutosha
 
Namuunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…