Bodi ya wadhamini Simba yapinga mkutano mahakamani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

si.jpg

Dar es Salaam. Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Soka ya Simba imefungua kesi kupinga mkutano mkuu wa klabu hiyo.

Mkutano mkuu wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.
Hata hivyo Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo wamefungua kesi hivi punde katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiiomba mahakama hiyo izuie kufanyika kwa mkutano huo.

Wakili wa bodi hiyo ya wadhamini, Juma Nassoro amelieleza Mwananchi kuwa kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa saa aaba mchana huu na Hakimu Thomas Simba.

Kabla ya kufikia uamuzi huo leo wa kufungua kesi, bidii hiyo ya wadhamini uliuonya uongozi wa klabu hiyo kuachana na mipango ya maandalizi ya mkutano huo na kwamba kama wakiendelea basi itakwenda mahakamani kuuzuia.

Uamuzi huo wa bodi ya wadhamini ni kinyume na kanuni za Fifa inayokataza masuala ya mpira kwenda mahakamani hivyo kuna uwezekano wa Simba ikapoteza nafasi ya kushiriki Ligi Kuu pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

mwananchi
 
Hivi kwenye mkutano mkuu huwa kuna nini, mbona kila timu hizi mbili Simba na Yanga wakiitisha mkutano mkuu wa timu kuna watu kama vile wanakosa amani, Wanaenda mahakamani.... Huwa kuna kutumbuana nini?

"A voice of one calling in the wildernes"
 
Club kwa maana ya viongozi , wanachama na mashabiki ndo walioshitakiwa na siyo club iliyoshitaki ; kwahiyo Simba haiwezi kuzuiwa kushiriki mashindano yoyote ya ndani wala ya nje .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwenye mkutano mkuu huwa kuna nini, mbona kila timu hizi mbili Simba na Yanga wakiitisha mkutano mkuu wa timu kuna watu kama vile wanakosa amani, Wanaenda mahakamani.... Huwa kuna kutumbuana nini?

"A voice of one calling in the wildernes"
Hapo kuna timu Mo na timu bodi ya simba ndo mvutano huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom