Bodi yakanusha uvumi kuwa walioomba mkopo wa elimu wanapaswa kujiandikisha upya...!!

Bodi yakanusha uvumi kuwa walioomba mkopo wa elimu wanapaswa kujiandikisha upya...!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.

Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.

Aidha Bodi inasisitiza kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni


mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: OLAS :Welcome au kupitia tovuti: Higher Education Students' Loans Board

Tangazo hili limetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji


BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU.


BODI YAKANUSHA UVUMI KUWA WALIOOMBA MKOPO WA ELIMU WANAPASWA KUJIANDIKISHA UPYA...!! - GUMZO LA JIJI
 
Back
Top Bottom