Bodi za Bandari na Shirika la Meli zitaundwa lini?

Bodi za Bandari na Shirika la Meli zitaundwa lini?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Tunaofuatilia utendaji wa mama kulinganisha na mtangulizi wake tulimsikia mama kwa mbwembwe huku akionesha ukali akitangaza kumtimua mwenyekiti wa bodi wa bandari na kuamuru bodi yake ivunjwe. Pia aliamuru kuvunjwa bodi ya shirika la meli linalomilikiwa na bandari.

Uamuzi huo aliuchukua baada ya kubainisha utapeli wa kutoa kandarasi ya ujenzi wa meli tano kwa kampuni hewa ya uturuki kwa gharama ya mabilioni hela za kigeni. Mama alisema baada ya uchunguzi wa siri 'due deligence' wa serikali waligundua madudu makubwa kwa madhumuni ya kuibia serikali.

Jambo linalokera na kutia mashaka hadi sasa inaelekea kama hakuna hatua zimechukuliwa kukidhi hatua ya uamuzi wa rais. Ni kipindi cha kama miezi mitatu tangu uamuzi wa mama lakini kimya kama giza titiri kimetanda.

Wengi tunaamini wezi na wahujumu wa umma waliokuwa wamelazimika kuteremsha silaha na kutulia wakipima upepo wamerejea kwa nguvu sehemu zote. Mama asipokuwa jasiri kufuatilia maamuzi yake kama kweli anamaanisha nchi itarudi kuchezewa na kuwa shamba la bibi kama kipindi cha nyuma.

Kwanza ujenzi wa meli maziwani umekua unafanywa na kampuni ya kizalendo songoro marines ambayo imeonyesha uwezo mkubwa wa nchi kujitegemea yenyewe kwenye eneo hilo. Kisa cha kupewa kampuni ya kituruki utaona ni wizi na ubadhirifu mtupu wa fedha za umma umerejea.

Wananchi tunasubiri kuona bodi mpya ya bandari. Tunajua hapo bandarini maslahi ya taifa huchezewa na kutishiwa na vibaka wa kiuchumi na kuna ma-agent wabaya dhidi ya nchi wa kila aina. Bandari wanahitajika watu weledi jasiri na wenye uzalendi mkubwa kusimamia.

Ni mategemeo tutasikia uundwaji wa bodi mpya ya bandari na shirika la meli karibuni.
 
Back
Top Bottom