historia inatumaliza sana, imetufanya tuwe wanyonge na tusijiamini hata kwa yale madogo tunayoweza kufanya.
- kutawaliwa kwetu na watu weupe kumetufanya hatuwezi kurudi katika asili yetu. wengi bado tunawaamini wazungu na waarabu kuwa wao ndio wenye akili na uwezo mkubwa na sisi tunawategemea wao na matokeo yake tumejikuta tukifanya yafuatayo:-
- kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa kupandikiziwa chuki, nakumbuka miaka ya nyuma ITV walikuwa wanaonyesha thamthilia au sijui sinema furani jina maarufu tulikuwa tunaiita kunta kinte hii picha natamani irudi tena sokoni japo kiukweli haiwezi kuwa na waangaliaji wengi kwakuwa kizazi tulichonacho hakipendi kufikiria sana kiko bize mno hivyo wao wakiangalia sinema za vita wasizozijua zimetokea wapi na nyingi zikieleza mazingira ya wazungu wanaona wamepata. kilichonivutia katika picha hii ni kuona wazungu wanaanza kupiganisha kuku kisha wanawapiganisha waafrika ikiwezekana mpaka mmoja afe halafu wao ndio furaha yao. sasa hii hakuna tofauti na sasa sema kwa sasa wanaiweka kwa maslahi ya uchumi zaidi.
- tumekuwa watu wa kujipendekeza sana kwa wazungu na tunaamini eti bila ya wazungu hakuna tunachoweza. miaka ya nyuma wakati nasoma shule ya msingi nilijengwa kuchukia tekinolojia ya kuiga kuwa haileti ufanisi lakini nilivyofika chuo na hapa ufahamu wangu ushakuwa mkubwa ndo naambiwa kuiga ndio kwa maana. nakumbuka masimulizi ya mtu mmoja wa karibu yangu wakati nyerere alivyotembelea banda fulani na kisha kwenda kwenye banda la SAHARA GROUP jinsi alivyoweza kuyatofautisha kwa jinsi gani Antony alionekana anafanya vizuri kuliko huyo mtu wakati huo na akimwambia hakuna jipya analolifanya hapa kila kitu umekopi hakuna ulichoongeza na unatengeneza under license hivyo huna jipya na hakutumia muda mrefu pamoja na kuwa na banda bora. ninachokitaka kusema tumekuwa tuko tayari kufanya chochote kile ili kumfurahisha mzungu hata ikiwa tutaathiri vizazi vyetu na mwisho wa siku wazungu huwa wanatucheka na kuendelea kutuita sisi maskini tunahitaji kusaidiwa.
- tumejengwa kwenye ubinafsi na ukatukaa kiasi kwamba hatutazami utu wetu ila makundi yetu. mimi ni mkatiliki kwa dini na kwa mpira mimi ni mshabiki wa Yanga katika vyama bado sipo popote, lakini makundi yanayofanana na haya yametutengnenezea uadui usio na maana tena afadhari haya vurugu zake sio kubwa lakini kwa ujumla wake kila kundi linajiona bora na kusababisha madhara kwa wengine kwa kujenga dharau na hapa ndipo hawa jamaa wanapotumia fursa za makundi haya kutujengea chuki na ubinafsi na kutugawa kisha wao kupora raslimali zetu.
- hatuoni shida mwingine kukosa na wewe peke yako ukakosa hata kama katika maisha yako hautavitumia vyote. mfano una umri wa miaka 60 unautajiri wa bilion 1000 ulioupata kwa kudhurumu wengine madawa ya kulevya na biashara zozote zilizotuumiza au kuwaumiza wengine hizi sinakusaidia nini ikiwa katika umri huo ukiishi sana ni miaka 20 lakini huku ukiandamwa na kisukari,pressure, na magonjwa mengine ya uzee? sisemi kuwa kila anayeumwa magonjwa haya ni mwizi hapana wengine yamechangiwa na hawa wezi kwa kujilimbikizia na kusababisha sononi na matokeo ya nje ndio hayo magonjwa. watawala wengi wamekuwa sio waaminifu na kusababisha mpaka leo haya yatupate.
- kutotambua thamani yetu kama watu binafsi,jamii,taifa na afrika kwa ujumla.
- wengi hatuna mipango na mikakati ya maana katika maisha yetu na wakati mwingine hatujui tunataka nini na kwanini na kwa muda gani na tufanyaje ili tufikie tunachotaka? matokeo yake tupo tayari kufanya chochote ikiwa na kuwa tayari hata kuatarisha maisha binafsi na ya taifa kwa ujumla kwa kuwa hatukujua mwisho kabla ya mwanzo. mtu haoni tabu kutoa siri za nchi kwa ajiri ya mkate wa leo ambao utasababisha yeye kutawaliwa siku zote.
- wapo watu kwenye jamii yetu wanamipango mizuri na wanaweza kubadilisha jamii lakini nao wamelemaa na kufanya kama wengine kwa kuwa na wao wamezoea kufanya kwa mazoea. matokeo yake wamekufa kwa uzinzi, ulevi wa kupindukia na stress za maisha huku ndoto zao au mawazo yao hayakupata fursa ya kutekelezwa na wao hawakuwa tayari kutafuta njia mbadala. mfano wasomi wetu wengi wanajua kuandika na kueleza umaskini wetu lakini imekuwa tabu kidogo kuleta tafsiri sahihi kwa tabaka linalokutana na hizo changamoto za kila siku wao wanaona poa tu kuwaandika wazungu wakalipwa fedha za kutosha wakawaacha wafrika wenzao maskini na sisi tukawazika wakiwa na elimu zao ambazo zimeishia kutuangamiza kwa wakoloni huku wao wakitumalizia ardhi yetu ya kulima kwa makaburi ya kifahari lakini yamehifadhi mifupa ambayo haikutumika wakati ikiwa hai na wamebaki kimya si kwa ukimya wa yai utatoa kifaranga hapana bali kwa mifupa mitupu inayosubiri baada ya miaka mia tatu mbele vitukuu vitapimiana viwanja chini ya hayo makaburi kwa kuwa uhitaji wake hautakuwepo lakini hebu angalia leo wale wasomi walioleta mabadiliko katika dunia bado tutawakumbuka. naamini kwame nkuruma itachukua muda kumsahau kwa mtazamo wake wa kutaka afrika iungane na hata gadafi kwa kutaka afirka ijipange kujitegemea. hivyo wasomi wajipange na wajipime kama thamani yao inakidhi mabadiliko chanya ya jamii.
- lmefika mahali lazima tujue nini tunaweza kufanya na nini hatuwezi na nani anaweza nini ili tujue kipi tunaitaji kujitegemea kama mtu binafsi,jamii,taifa na afrika kwa ujumla ili raslimali zilizopo zitumike kwa waafrika kwanza na sivinginevyo nawapenda wachina hata kama wao hawawezi wakitengeneza kinachofanana watakibadilisha jina kutoka mfano nokia wao watakita nakia kabla ya kesho kuja na bland name yao mtakayoikubali inayoitwa ho! sasa nafikiri tufike huko pia.
- tumekubali kugawanyika kwa kuwa vibaraka kwa sababu eti ya kuwambiwa sisi ni maskini wa kutupa utafikiri wao hakuna wanachohitaji kwetu. taifa la Israeli kwa kadri ya masimulizi ni watu waliopigana vita nyingi sana na shida nyingi sana na hili limewafanya wao kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri na kutawala na muda mwingi hawakuwa na mali nyingi na hata nchi yao pia haikuwa kubwa katika ardhi lakini kwa uvumilivu huo leo wako mbali. hata china nao kuwa tayari kuvumilia na kutumia vizuri soko la ndani na taifa kufundishwa kutumia vya ndani kumesaidia sana kuwa taifa kubwa na kwa sasa wanatawala uchumi wa dunia ambao marekani wanawaogopa kwa kuwa wako mbali sana na hii ni kutokana na uwekezaji wa muda mrefu waliofanya afrika sasa leo wamarekani wanatutumia na sisi tunawaona wamaana sana shame upon us!
yapo mengi ya kuongea lakini kwa bahati mbaya wengi hawapendi kusoma mambo marefu labda tuangalie nini tufanye japo inaweza kuchukuwa muda lakini bora tuchelewe lakini tufike:-
- lazima tujivue utumwa na kutokukubali kubuluzwa na kupelekeshwa na weupe kisa walitutawala
- tofauti zetu za makundi zisisababishe tukachukiana na kutodhamini utu wetu na hapa watu wa mbagala wanakwambia hasara roho fedha makaratasi yani tusiwe tayari kufedheheka kwa jaili ya fedha chache ambazo hazitufikishi kokote.
- kila mmoja awe tayari kufanya mabadiliko yake binafsi, familia,jamii na taifa kwa ujumla ili tuwe na dira itakayotupeleka tunakotaka kama taifa na afrika kwa ujumla.
- lazima afrika tuchague viongozi tunaoamini wanaweza kusimamia maslahi ya afrika na sio wanaoweza kuuza bara letu kwa maslahi yao binafsi, bora tuumie kwa muda mrefu lakini kuwe na uelekeo tunaouamini.
- tufikirie jinsi ya kumaliza migogoro yetu ya ndani kwa majadiliano tukijitegemea wenyewe kiukweli huwa sielewi tukipisha kidogo hao kwa wazungu kiukweli naamini wanatucheka
- lazima tutengeneze viongozi toka wadogo na sio hawa tunaowekewa na wazungu.
- tutumie vizuri soko la ndani kwa bidhaa zetu na kisha tujenge uchumi imara kwa maslahi yetu
yapo mengi lakini kwa kifupi tunahitaji kujitazama upya tukijenga uchumi imara kwakuwa ndio chanzo cha migogoro yote hii na tusikubali kugawanyika katika misingi ya dini kwa jinsi yoyote ile kwa kuwa vita ikiunganishwa na dini inakuwa ngumu zaidi nadhani mnakumbuka ile vita baridi ya uchinjaji wakristo walivyogoma kula nyama buchani nini kilitokea lakini mwisho busara zilitumika na tukaendelea kuelewana.