BOLT amkeni , madereva wenu wameanza kuwa matapeli na wameanza kuwachafua

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Dereva siku hizi anazima data akifika mbele anajifanya haoni kitu kwa System so anataka mkadiriane bei. Mwingine zile discount za mteja mpya wanakataa wakidai Bolt ofisi zimefungwa hapa nchini.

Kuna wakati kama mtumiaji hajielewi au haijui sehemu , dereva anachukua simu ya mteja kama anamsaidia, halafu anaweka location ya mbele kidogo yaani ili azidi hata 500.

Yeyote aliyepigwa au kukutana na magumashi ya waendesha Bolt aweke hapa:
 
Mkuu kama taifa nadhani tuna mambo mengi mno ya kulalamika kwenye hili taifa letu mengine haya sijui bolt ni ya kuyapotezea tu.Hivi kwa akili yako unadhani bolt imewaajili wale vijana?kwa taariafa yako ni kwamba wale vijana ndio wanamlipa bolt kwa makubaliano waliokubaliana sasa wakati mwingine hao bolt na app zinazofanana na hizo huwa wanajitoa ufahamu kwa kumjali zaidi mteja wakati upande wa pili wanamuumiza dereva ambae kimsingi huyu ndio mtu muhimu sana kwa mustakabali wa usafiri.
 
Katika hali ya kushangaza hao unaowaita bolt hawana ofisi kaa wala mkurugenzi wao hajulikani ni nani kaa ukilijua hilo kwa mazingira hayo ni vigumu kuhakika matatizo yenu au ya hawa madereva yanasikizwa au kutatuliwa na ndio maana madereva wanaamua kujiongeza kwa kufanya mambo wanayoweza ili angalau familia zipate chochote kitu.

Madereva hawa wanahali ngumu sana ni vile wewe hujui tu labda sababu watanzania wengi wanapenda vya mteremko zaidi nikupe mfano mdogo tu unaambiwa umchukue mtu pale makumbusho na umpeleke kimara mwisho kwa shilingi elfu 4😆 we bro hivi kwa mazingira hayo kwako ni sawa?au umtoe mtu taifa umpeleke kigogo ya mburahati kwa elfu moja na mia tano?🤭Angalia mazingira hayo tu kwanza alafu tafakari mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…