KERO Bolt Tanzania iweke njia rahisi na za uhakika za kupata msaada Mwanza, hawana hata ofisi

KERO Bolt Tanzania iweke njia rahisi na za uhakika za kupata msaada Mwanza, hawana hata ofisi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaiomba Bolt kuboresha huduma kwa wateja jijini Mwanza kwa kuanzisha ofisi ya huduma kwa wateja au kuweka njia rahisi na za uhakika za kupata msaada.

Wateja na madereva wa Bolt tumekuwa tukikabiliwa na changamoto mbalimbali, lakini tunapojaribu kuwasiliana na kampuni hiyo, mara nyingi tunaelekezwa kwa roboti ya AI ambayo haitoi msaada wa kutosha kutatua matatizo yetu. Hali hii inakuwa ngumu zaidi kutokana na kutokuwepo kwa namba ya simu ya huduma kwa wateja.

Changamoto hii haiwahusu wateja pekee, bali hata madereva wa Bolt jijini Mwanza, ambao nao wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa ofisi au huduma yenye ufanisi ya kushughulikia matatizo yao.

Tunaomba Bolt ichukue hatua za kuboresha mawasiliano na huduma kwa wateja na madereva wake, ili waweze kupata msaada wa haraka na wa kuridhisha wanapokabiliwa na changamoto.
 
Back
Top Bottom