Boma la hii ramani litagharimu kiasi gani?

EricMan

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2017
Posts
3,050
Reaction score
5,420
Wakuu Salaam kwenu
Kwa mimi nikapanga hivi
Tofali 2500 @ 1100 = 2,750,000
cement 50 @ 16,000 = 800,000
Mchanga fiat 2 @ 150,000 = 300,000
Nondo sjapata maesab ila naiwekea 1M
Ufundi. 2,500,000

jumla ni kama 7,350,000~ 8M

Wakuu 8M boma si linaisha bila utata wowote?

Nakarbisha Maoni, critics n.k
 
8m boma? Bro una Utani na Ujenzi asee
 

Eneo likoje?
Huwezi kusema mfano tofali 2,500 kama topography ipo sloped, lazima zitakuwa nyingi zaidi, ndio maana huwa tunauliza topography ya eneo. Mimi naona kabisa tofali (japo hakuna vipimo) hazipungui 3,000.

Si tunafanya rough estimates, basi cement weka walau 60 bags.

Mchanga ni sawa, fuso mbili.

Kokoto fuso moja kwa ajili ya mkanda wa chini na juu.

Nondo kwa wastani ziwe nusu tani(42-45pcs)

Ufundi ni variable kutegemea na eneo.

Bati 100+, upauaji utategemea unachukua bati za aina gani hivyo mbao na ufundi wake pia ni variable. Kwenye kupaua huwa gharama utaamua wewe kutokana na a) aina ya upauaji, b) quality ya bati unayonunua, c) utaalam wa fundi nk. Kuna anayepaua kwa 15m na nyumba hiyo hiyo mwingine anatumia 25m..choices za ubora!
 
Mzee achana na hao
Hilo Jengo linaisha tena bila shida utashangaa mtu anakuja kukwambia eti mil100
Sijui watu wa mjini wanajenganga kwa kutumia nini mtu anakuambia bei kubwaa utasema anajenga kwa kutumia dhahabu wakati sisi huku gharama kubwa ni kwenye mabati na kenchi zake huku kwingine kuanzia chini mpaka lenta mbona oya oya tu
 
na mm nalenga hapo chini mpaka lenta bas kwa 8M kuna mtu kasem sitobii
 
Unachosema ni kweli ila ubora wa nyumba zetu unauonaje?

Tunatumia gharama ndogo kwa sababu tu hatuna pesa, ila kusema kweli nyumba nyingi zipo substandard. Likija mfano tetemeko dogo tu la richter scale ndogo tu hapa Dar ndio tutajua aina ya ujenzi tunaojenga.
 
Point
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…