Boma la hii ramani litagharimu kiasi gani?

Linasimama ila umesahau kokoto
 
Ukizungumzia tetemeko basi ujue nyumba nyingi hata hiyo unayofikiri umeijenga kwa gharama lazima itembee nakuhakikishia
 
Ndio witty, yeye aende site na hiyo 8m mkononi, aanze na foundation....akishafunga mkanda atapata majibu kama inatosha au aongeze, ila hapo tayari msingi utakuwepo.[emoji28][emoji28]
Hapo sawa...
 
Sijaona bajeti ya mbao, bajeti ya ufundi tangu chini mpaka kupauwa bajeti ya milango na madilisha pia bajeti mfumo wa maji
 
Kuna watu watakupinga lakini hiyo gharama uliyoitaja ndio ukweli, hata kama itapungua basi si chini ya million 13
 
ml 8 mpaka leta nyingi sana mkuu na chenji inabaki mkuu
 
Makadrio yyte atakayokuambia fundi usiamini , weka mara mbili yake utakuja kunishukru badae nimekaa pale
Nakoleza wino kabisaaaa,kuna fundi nilitamani kama kupiga walahi tena daaa,makadirio tulifanya wote na sehemu nyingine nikashauri tuongeze kilichotokea mbele ya safari...Mungu anajua aiseee
 
Kujenga ni ishu bila 20M apo sitaend popot. hawa mafund sio w kuwaamin kiviile
Nilianzisha ujenzi baada ya fundi kufanya tathmini na kuniambia estimated cost ni kama 12M mpaka usawa wa renta, tulivyoanza ujenzi mpaka kufikia renta n'a kujenga shimo la choo, ilikuwa imekata 23M, nilipomwambia fundi mbona makadirio yako feki akaniambia "bro nilijua kabisa itafika huku, ila ningekwambia pesa zote hizi nakuhakikishia usingejenga, lakini sasa umeweza jambo ambalo ulidhani hauwezi"

Nilikasirika lakini moyoni nilimkubali sanaaa, maana alifanya kila shilingi niliyopata niielekeze pale, otherwise hakika nisingejenga kabisaa!
 
hapo najiwekea mwenyew sebule 5 kwa 4 vyumba 3 kwa 3 vyoo 1.2 uko pale kichen bawek 3.4 kwa 4 uko kwengine patajiset tu fundi akiiangalia [emoji23]
Aisee mbona unataka kujenga size za kizamani? Sebule ya 4x5 ni ndogo angali 6x6. Kumbuka unajenga nyumba itakayodumu kwa miaka 30 ijayo

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…