Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,386
- 5,325
BOMBA LA MAFUTA LA AFRIKA MASHARIKI: DIPLOMASIA YA UCHUMI YA URITHI WA JPM NA MAPATO YA TSH 76.32bn KWA MWAKA
Mnamo Septemba 27, 2020 Uganda na Tanzania ziliingia makubaliano kupitisha Bomba la Mafuta ya Afrika Mashariki kutokea Hoima (Uganda) hadi Bandari ya Tanga (Tanzania). Hii ni moja ya mafanikio makubwa ya Diplomasia ya Uchumi ya Hayati JPM. Maana iliua kabisa ndoto za Kenya kupitishia bomba hilo kwenda Bandari yake ya Lamu.
Mradi huu ni alama ya urithi itakayo ihakikishia Tanzania kiasi cha $12.7 kwa kila pipa litakalo safirishwa katika bomba hilo kutokea Uganda.
Hivyo kibiashara na kiuchumi, huu ulikuwa ni ushindi wa kimkakati kwa Tanzania wenye uwekezaji wa takribani $3.6bn na zaidi ya asilimia 70 ya bomba litapitia Tanzania hivyo itakuwa imevutia kiasi kikubwa cha uwekezaji kutoka nje kati hizi $3.6bn.
Bomba hili linatarajiwa kupitisha pipa la kwanza mnamo 2025. Na kwa siku yatasafirishwa mapipa 216,000 ya mafuta ghafi. Hii itaihakikishia Tanzania takribani $2.743 mil (Tsh 6.36bn) kwa siku. Hii ni sawa na $32.92mil (Tsh 76.32bn) kwa mwaka kama tozo ya kusafirishia mafuta hayo. Haya ni mapato mapya.
Kuna kama mapipa 6.5bn ambayo yamekwisha thibitishwa huko Uganda katika visima Kingfisher na Tilenga. Hivyo Tanzania itakuwa na uhakika wa kutengeneza mapato mengi zaidi kwa takribani miaka 30 ijayo kutokana na Mkataba uliohitimishwa siku ya Jumapili tarehe 11 Aprili 2021 wakati Rais Samia Suluhu Hassan aliposhuhudia utiwaji wa mikataba hiyo ya kimkakati. Kazi inaendelea. Huku Rais Yoweri K. Museveni akisema siku huyo ilikuwa ni siku ya Ushindi wa aina Tatu (Kitiva, Kisiasa na Kiuchumi) kwani Tanzania imekuwa sehemu ya kupigania ukombozi wa Uganda kutoka wa mikono ya Idd Amini pamoja na ukombozi wa bara la Afrika. Hivyo hii pia ni sababu iliyorahisisha uamuzi wa kuifanya Tanzania kuwa njia ya kusafirishia mafuta hayo ili Tanzania nayo ipata kitu kutokana na majotoleo yake katika Ukombozi wa Afrika.
Ndiyo maana ninaamini kuwa hapa JPM aliacha legacy kubwa..na ni ushindi kwa Tanzania katika Diplomasia ya Uchumi katika Afrika Mashariki dhidi ya Taifa lenye Uchumi mkuwa kwa sasa katika Ukanda huu.
Ninaamini pia faida zitakuwa ni nyingi zaidi ya tozo hii ya $12.7 kwa kila pipa litakalosafirishwa kwa siku. BOMBA hili kitakuwa linapashwa joto ili mafuta hayo ghafi nyenye mnato mkubwa (viscocity) yaweze kupita. Ninaamini kwa kuwa na Umeme wa uhakika pia tutapata mapato ya ziada yanayoweza kusaidia kurejesha fedha nyingi zilizowekezwa katika vyanzo vya Umeme hada bwawa la JNHPP-2115MW. Faida nyingine ni Ajira za muda mfupi na muda mrefu zinazofikia elfu kumi (10).
Lakini Prof Assad hana impact hata kwenye ukoo wake.