Tatizo ni viongozi wetu, hasa decision makers, aidha out of
ignorance or greedy wameshindwa kufanikisha mapinduzi ya viwanda Tanzania; badala ya kukabiliana na wawekezaji ili uwekezaji uwe na manufaa kukuza sekta yetu ya viwanda, wao wanaendelea tu kuwakenulia wawekezaji, kwani wanajua fika akaunti zao za Uswisi zitazidi kuwa kubwa, huku vipato vya watanzania walio wengi vikizidi kunyauka;
Hakuna Taifa lililo fanikiwa kuendeleza Viwanda kwa kutegemea nguvu za soko peke yake, na ndio maana hata Mwalimu Nyerere alifanikiwa kwa sababu kulikuwa na mkono mzito wa serikali; Kuna maeneo mengi ambayo soko huwa linafeli, hivyo yanahitaji mkono wa serikali, kwa mfano maeneo kama utafiti, miundombinu ya tekinolojia na mawasiliano, nishati, risk finance, skills, n.k, ambayo soko peke yake haliwezi kuwekeza kwa ufanisi kwani mengi ya haya yanahitaji gharama kubwa, hasa iwapo uwekezaji huu unalenga kwa wananchi walio wengi – vijijini; Soko halioni faida ya kufanya hivyo, na isitoshe, ni gharama kubwa sana ambayo ni serikali tu ndio inaweza kuibeba; Tatizo lililopo ni kwamba, sera za uliberali zinaibana serikali isifanye haya, ingawa iwapo serikali ingeamua kuwa kali kidogo, hasa kwa kuanzisha mikakati ya kujitegemea kupitia rasilimali tulizojaliwa na Mungu, na kuachana na utamaduni wa kutembeza bakuli la misaada, tungefanikiwa katika hili;
World Bank, IMF, na nchi wahisani wamekuja na Rules of the game chini ya uliberali, ambazo zinakataza serikali kujiingiza katika uwekezaji wowote mkubwa kwenye uchumi, zaidi ya matumizi ya hapa na pale kwenye sekta za afya, elimu ya msingi, sekondari kidogo, miundo mbinu na maeneo machache ambayo hayatishii interests za wakubwa; Hata kwenye suala la elimu, lengo sio
ELIMU BORA, bali
BORA ELIMU, ndio maana wanasiasa wetu uchwara ndani ya CCM wanaitikia kwa kufunua kinywa chote Ubeti wa Nyimbo za wahisani kuhusu mafanikio ya Elimu Tanzania, kama vile High Enrollment Rates, lakini suala la nini kinafuata baada ya hizo explosives enrollment rates in terms of learning outcomes za watoto wetu na uhusiano wake na mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya uchumi kwa ujumla, wimbo wa namna hiyo haujatoka bado;
Wanasiasa wetu wana tabia ya kujipongeza sana kwamba kuna inflow kubwa ya FDI Tanzania, kuliko nchi nyingine zote za Afrika Mashariki n.k, lakini wanajisahau kwamba FDI zenye manufaa kwa taifa ni zile ambazo kwanza – haziji kununua mashirika yetu ya umma na kuyafanyia
assest stripping na kuondoka zao kama TRL; wanajisahau kwamba FDI zenye manufaa kwa taifa sio zile zinazokuja kutafuta management contracts kama Tanesco na TTCL, na kukimbia wakishapata chao; Wanajisahau kwamba FDI zenye manufaa kwa taifa sio zile zinazokimbilia kwenye Rasilimali zetu (madini) na kuzichimba na kubeba bila hata ya kufanya any vale addition kwenye uchumi wetu in terms of creating value chains and supply chains za maana ambazo zingetoa ajira, zingetoa fursa kwa wazalishaji wazawa kutengeneza bidhaa zinazohitajika kwenye sekta hii n.k; Badala yake, kwenye suala la madini, wawekezaji wanakuja na kila kitu – kuanzia caterpillar, screw drivers za kufanyia matengezo, na hata mafundi, mfano kampuni ya Mantrak Tanzania…
Ndio maana leo uchumi wetu unakua lakini maisha ya watanzania yanazidi kuzorota kwani wananchi walio wengi, hasa vijana, hawana ajira, hivyo kusumbuliwa na inciome poverty, Wenye vipato ni wanasiasa wanaopewa 10% kwa kila miradi hii ya kinyonyaji;
Tunachohitaji ni FDI zinazoenda kwenye manufacturing sector na kwa maelezo na maelekezo ya serikali chini ya effective industrial policy kwani kwa kufanua hivyo, FDI hizi zitaleta faida nyingi kama vile technology spill over, technology transfer n.k; Nchi zote za East Asia ambazo zilifanikiwa na Maendeleo ya Viwanda zilifanya hivyo kwa kukaidi rules of the game chini ya uliberali, na ndio maana World Bank na IMF huwa wanajikanyaga na kuwa waangalifu sana wanapotumia nchi kama South Korea kama a success story; South Korea, Taiwan, Singapore, China zote zilienda kinyume na World Bank na IMF, na taasisi hizi miaka ya sitini na sabini, zilipinga sana sera za uchumi katika nchi hizi na kuonya zitaporomoka; Ni nchi moja tu ndio iliwasikiliza wakubwa hawa – Hong Kong, na matokeo yake ni kwamba, Hong Kong ilifanikiwa kuendelea kwa miaka michache, lakini by 1990s na hadi sasa, Hong Kong imekuwa one of the a ‘classic failures' under the watch of the World Bank and IMF;
Tanzania tunaweza kufanikiwa iwapo tutajifunza kutoka kwa weznetu; Ili kufanikiwa, kuna maeneo mengi muhimu ya kuzingatia ikiwa ni pamoja na haya matatu:
- Development of Skill Base – kupitia elimu, na uwekezaji kwenye utafiti na ubunifu, na hapa ndio suala la National Innovation Systems pia linaingia, suala ambalo mpaka leo hii, Wizara ya Sayansi na Tekinolojia wala haina habari juu ya umuhimu wa National Innovation Systems kwa taifa; Kuna Naibu Waziri kijana pale, pengine atabadilisha hili;
- Export Promotion Strategy ambapo Manufacturing Value Added as a percentage of GDP ni muhimu iongezeke sambamba na Export of these Manufactured products - as a percentage of GDP;
- Na tatu ni Macro Economic Management – masuala ya controlling inflation, unemployment rates, enhance economic growth with benefits that trickles down to the poor, na maeneo mengine muhimu yaku-stabilize uchumi on the macro level;
Kitu kinginge muhimu sana katika mafanikio ya viwanda ni kujenga our own
TECHNOLOGICAL CAPABILITIES, lakini kama tulivyojadili, hatuwezi kujenga hili kwa kutegemea nguvu za soko peke yake, kwani soko halina muda na kuja kujengea mtu uwezo huo, bali lipo tayari kuja to take advantage of the existing capabilities, kama ilivyotokea Singapore, China n.k; Pia serikali inabidi kujenga supporting industries ambazo zitakuwa ni sehemu ya Value chains and supply chains ya Viwanda Mama vitakavyoletwa na FDI – hasa katika manufacturing sector itakayoambatana na technology transfer & spillovers kama tulivyojadili hapo juu; Yote haya ni maeneo ambayo Serikali inatakiwa iyafanyie kazi, sio nguvu za soko, kwani soko huwa linafeli katika mengi ya haya; Muhimu hapa pia ni yale maeneo tuliyojadili ya serikali kufanyia pia kazi, hasa suala la factor markets kama vile - skills development, risk finance, tech infrastructure,
market information, n.k;
Viwanda Wakati wa Ujamaa
Tanzania ilifanikiwa sana katika eneo hili, hasa kipindi cha 1970 – 1977 ambapo production capacity ya viwanda vyetu ilikuwa over 70%; hiki ni kiwango cha juu sana; Lakini kutokana na sababu mbalimbali, kuanzia miaka ya mwishoni ya 70, hii capacity ikaanza kuporomoka na hatimaye kufikia karibia 40% kufikia mwaka 1984; Kuna sababu nyingi zilizopelekea kuporomoka kwa viwanda vyetu, na tumeshajadili hizi kwa kina; Lakini hapa ningependa kuongezea suala la
infant industry protection policy (sera ya kukinga viwanda vya nyumbani dhidi ya ushindani kutoka nje); Sera hii ilitumika sana chini ya Import Substitution Strategy wakati wa Ujamaa;
Pamoja na umuhimu wake, infant industry protection ilifanywa kwa uholela kwani – sera hii ililenga Viwanda vyote Tanzania badala ya serikali kuwa SELECTIVE na baadhi ya viwanda ambavyo vilikuwa vinahitaji protection, huku ikiacha vile ambavyo vilikuwa na uwezo ili vishindane na bidhaa kutoka za nje/nchi jirani kama Kenya na kuzidi kujiimarisha; Serikali ilitakiwa ifanye SELECTIVITY katika hili; Vinginevyo, sera ya kukinga viwanda vyote bila ya selectivity ilichangia sana kwa viwanda vyetu kukosa ari ya ubunifu, ujenzi zaidi wa capabilities n.k, kwani "come what may, serikali ilikuwa ipo kwa ajili yao" matokeo yake yakawa ni kuanguka kwa efficiency, kuongezeka kwa ubadhirifu n.k; South Korea Serikali yao iliweka mikakati mingi sana ya kuzuia hili, ikiwa ni pamoja na performance indicators mbalimbali…
Protection ya viwanda vya nyumbani dhidi ya ushindani kutoka nje itafanikiwa iwapo tu viwanda hivyo kweli vinahitaji protection, au iwapo vile vyenye uwezo wa kushindana vinapata competition kidogo kwani hii inavifanya viwekeze zaidi kwenye capability building; Lakini tufahamu kwamba katika mazingira ya sasa, ni vigumu sana kwetu sisi kufanikisha Maendeleo ya viwanda bila kujipanga vizuri, hasa kutokana na uwepo wa China na mataifa mengine mengi ambayo yametupita sana kutokana na wao kuwekeza kwa muda mrefu katika maeneo tuliyojadili hapo juu; Mafanikio yetu yatapatikana iwapo viongozi wetu wataamua kuwekeza kwa faida ya vizazi vijavyo, lakini kwa mwendo huu wa wanasiasa wetu kukimbilia miradi ya zima moto au ile ambayo wanataka waone inafanikiwa na waache Legacy wakiwa bado HAI, hakika HATUTAFIKA;
Umuhimu Wa Sekta Ya Kilimo
Katika hoja yangu yote hapa sijataja Kilimo lakini haina maana kwamba hakina maana; Kilimo ndio nguzo yetu kuu ya kufanikisha yote haya, hasa iwapo tutalenga Mapinduzi ya Kilimo kwa dhati, na sio Kilimo Kwanza ambayo imekaa kisiasa zaidi; Bila ya Kilimo, itakuwa ni vigumu kwa nchi yetu kufanikiwa kuendeleza Viwanda kwani sekta hizi zinategemeana, na hakuna nchi iliyofanikiwa na viwanda kwa kupuuzia Kilimo; Tunachohitaji ni kuongeza Producutivity kwenye kilimo na vile vile mapato ya wakulima, na tukifanya vizuri, hasa katika GDP yenye thamani nzuri pamoja na exports, tutakuwa kwenye nafasi bora zaidi ya kupata fedha za kuwekeza kwenye sekta ya viwanda pole pole sambamba na sekta ya kilimo, na pole pole, viwanda vitaanza kuongezeka (processing factories, light manufacturing and eventually heavy manufacturing) in the long run; Isitoshe, Joseph Stiglitz, moja wa wachumi bora duniani alipata sema kwamba:
"It makes no difference whether the economy produces potato chips or computer chips, the economy should produce whatever maximizes GDP."
Tukifikia hatua ya kuwa na viwanda vya kutosha, huku kilimo nacho kikiendelea kulipa in terms of income kwa wakulima, sekta hizi pole pople zitaaza kugawana jeshi la ajira, and in the long run, sekta ya viwanda pamoja na value chains zake zile immediate lakini pia the sector servicing it, zitazidi kukua, na hivyo kusaidia dependency ya ajira kwenye sekta ya kilimo kuanza kushuka na baadae kuwa insignificant, huku vijana wakihamia kwenye industrial and service sectors; Lakini ili kufanya ajira kwenye kilimo iwe INSIGNIFICANT BAADAE, NI LAZIMA KUIFANYA IWE SIGNIFICANT LEO, kupitia an effective industrial policy kama tulivyojadili;
Umuhimu Wa Sekta Ya Madini
Nje ya Kilimo kama njia ya kupatia taifa mitaji kuwekeza kwenye viwanda, pia kuna sekta ya madini na mafuta ambazo tunaweza kuchuma huko na kupandikiza kwenye viwanda; Lakini bila ya uangalifu, sekta za madini na mafuta zinaweza kutupeleka kubaya kuliko sekta ya kilimo katika kutuendeleza kuwa taifa la uchumi wa viwanda; Ni nchi chache sana duniani zimefanikiwa kuingia katika mapinduzi ya viwanda kwa kutegema rasilimali za madini na mafuta, hivyo ni muhimu tukatambua hili na kuacha siasa za kudanganya wananchi; Hakuna kisichowezekana, lakini ni muhimu tukatambua changamoto zilizopo;