Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Boniface Jacob, akizungumza katika mkutano wa hadhara Viwanja vya Soko Kuu jijini Arusha amesema kuwa ili kukomesha vitendo vya utekaji na mauaji holela vinavyoendelea nchini, Serikali inapaswa kupiga marufuku askari wa Jeshi la Polisi kufanya ukamataji bila kuvaa sare rasmi za jeshi hilo.
Soma Pia: Simbachawene: Ya nini uende kumkamata mtu nyumbani kwake umevaa kininja? marufuku polisi wasiovaa sare kukamata watu
Aidha, amesema Jeshi la Polisi linapaswa kupigwa marufuku kutumia magari yasiyo rasmi wakati wa ukamataji, akieleza kuwa askari wanapotumia magari binafsi na kutokuwa na sare rasmi, inakuwa vigumu kwa wananchi kufahamu mtu aliyekamata ni nani.