Bondia Cheka atoroka darasani Morogoro,ataki kurudi tena shule

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
“Sijui kwa nini Cheka hataki tena kwenda shule, tangu alipopewa nafasi alikwenda mara mbili tu kujisajili na kupiga picha lakini kusoma hajawahi,” mama huyo ameiambia Mwanaspoti mjini Morogoro.

BINGWA wa Dunia wa WBF, Francis ‘SMG’ Cheka hajawahi kuingia darasani hata mara moja tangu alipopewa nafasi ya kusoma kwenye Chuo cha St. Joseph huku mama yake mzazi, Merry Raphael akidai amemuhimiza aende shule mpaka amechoka.

“Sijui kwa nini Cheka hataki tena kwenda shule, tangu alipopewa nafasi alikwenda mara mbili tu kujisajili na kupiga picha lakini kusoma hajawahi,” mama huyo ameiambia Mwanaspoti mjini Morogoro.

Merry, ambaye ameiarifu Mwanaspoti kuwa Cheka ni mtoto wake pekee alibainisha kuwa amemshauri kijana wake huyo suala la kwenda shule ambalo limeonekana ‘kizungumkuti’ kwa Cheka huku akidai kuwa nafasi hiyo haitajirudia kwa mwanae huyo.

Cheka alipewa ofa hiyo ya kimasomo baada ya kutwaa taji la WBF Agosti 30 kwa kumchapa kwa pointi bondia wa Marekani, Phil Williams na kutakiwa kuchukua masomo ya Kiingereza, kompyuta na biashara.

Mwanaspoti ilifika chuoni hapo maeneo ya Kihonda, Morogoro na kukuta wanafunzi wenzake wakiendelea na masomo huku mwalimu anayemsimamia Cheka, Lameck Mkissi akidai bondia huyo hajawahi kuingia darasani hata siku moja. “Tumejaribu kumtafuta bila mafanikio, sasa hata simu zetu hapokei, alichokifanya ni kuja na kujaza fomu na kupiga picha kwa ajili ya usajili alipoondoka hakurudi tena karibu mwezi sasa, wenzake wanaendelea na masomo,” alisema mwalimu huyo.

Hata hivyo Cheka alieleza kuwa bado anajipanga na wakati wowote atakwenda kuanza masomo yake huku akibainisha kuwa alishindwa kutokana na matatizo ya kifamilia.

“Unajua mimi ni baba na familia inanitegemea kwa kila kitu hivyo nitakapoanza kwenda shule lazima nihakikishe kila kitu kinakwenda sawa hapa nyumbani kwani nikiwa kule mambo yangu mengi yatasimama,” alisema bondia huyo baba wa watoto wawili, Boniface na Historia.
 
heri atoroke tu,maana sipati picha walimu wangekuwa wanafundisha kwa mashaka,maana jamaa akimind utakwepaje ngumi jiwe
 
the business is done....nigga is bak on street grindin
 
Unazani akili itatumia maguvu kuelewa Area of a siko ekwoz to Pai times radius skwea?
 
Nilimtakia mema sana, lakini kashindwa. Sasa tufanyeje?

Ingekuwa kupambana na kwa maguvu najua angejaribu, lakini kusoma?! Ni kipaji na kila mtu anacho.

alipotangaza kwenda kusoma we Kongosho ulimpongeza sana
 
vitu vingine wala haviitaji kuumiza kichwa watu wanapewa udokta hata sindano hawajui kushika sembuse maudhulio darasani? y take point ni kama bibi anamwimiza mwana aende shule sijui kwa mjukuu itakuwaje?
 
Alishindwa dogo Mr Bluu sembuse Cheka baba wa watoto?
 
daa jf raha tupu.nimecheka sana daaa
hahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…