Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Sijui kwa nini Cheka hataki tena kwenda shule, tangu alipopewa nafasi alikwenda mara mbili tu kujisajili na kupiga picha lakini kusoma hajawahi, mama huyo ameiambia Mwanaspoti mjini Morogoro.
BINGWA wa Dunia wa WBF, Francis SMG Cheka hajawahi kuingia darasani hata mara moja tangu alipopewa nafasi ya kusoma kwenye Chuo cha St. Joseph huku mama yake mzazi, Merry Raphael akidai amemuhimiza aende shule mpaka amechoka.

Merry, ambaye ameiarifu Mwanaspoti kuwa Cheka ni mtoto wake pekee alibainisha kuwa amemshauri kijana wake huyo suala la kwenda shule ambalo limeonekana kizungumkuti kwa Cheka huku akidai kuwa nafasi hiyo haitajirudia kwa mwanae huyo.
Cheka alipewa ofa hiyo ya kimasomo baada ya kutwaa taji la WBF Agosti 30 kwa kumchapa kwa pointi bondia wa Marekani, Phil Williams na kutakiwa kuchukua masomo ya Kiingereza, kompyuta na biashara.
Mwanaspoti ilifika chuoni hapo maeneo ya Kihonda, Morogoro na kukuta wanafunzi wenzake wakiendelea na masomo huku mwalimu anayemsimamia Cheka, Lameck Mkissi akidai bondia huyo hajawahi kuingia darasani hata siku moja. Tumejaribu kumtafuta bila mafanikio, sasa hata simu zetu hapokei, alichokifanya ni kuja na kujaza fomu na kupiga picha kwa ajili ya usajili alipoondoka hakurudi tena karibu mwezi sasa, wenzake wanaendelea na masomo, alisema mwalimu huyo.
Hata hivyo Cheka alieleza kuwa bado anajipanga na wakati wowote atakwenda kuanza masomo yake huku akibainisha kuwa alishindwa kutokana na matatizo ya kifamilia.
Unajua mimi ni baba na familia inanitegemea kwa kila kitu hivyo nitakapoanza kwenda shule lazima nihakikishe kila kitu kinakwenda sawa hapa nyumbani kwani nikiwa kule mambo yangu mengi yatasimama, alisema bondia huyo baba wa watoto wawili, Boniface na Historia.