Bondia Dula mbabe wa Tanzania ashushiwa kichapo kizito huko Uk

Huyu mbabe nae ashakua kama mandonga sasa, maneno mengi akiingia ulingoni deile anagongwa.
Huyu ni mla ugali dona toka uzaramuni, pesa yote anayopataga huwa anaiwekeza katika ugali dona na tembele la kuchuma, kwa kifupi jamaa ni mganga njaa anaeendesha maisha yake kwa kupigwa ulingoni
 
Nimeangalia hili pambano, yani ni kama Mtibwa vs Liverpool.

Dulla alikua anarusha ngumi hovyohovyo kama mlevi na kuacha uso wazi.

Halafu alikua mchafu, bukta lenyewe kubwa halimtoshi mpk kalikunja kiunoni kama dera, sijui nani kamvalisha.
 
Nimeangalia hili pambano, yani ni kama Mtibwa vs Liverpool.

Dulla alikua anarusha ngumi hovyohovyo kama mlevi na kuacha uso wazi.

Halafu alikua mchafu, bukta lenyewe kubwa halimtoshi mpk kalikunja kiunoni kama dera, sijui nani kamvalisha.
Dula mbabe ni kituko, siku moja, kabla ya pambano lake na bondia katompa kutoka congo, jamaa alikuwa kwenye harusi uswahilini, akakesha anakula mapilau na minyama plus misoda akavimbiwa kesho yake akawa anasinzia hovyo ulingoni, alipigwa ngumi kama 16 zakidevu akatema maji, ndo ikawa baba jeni bye bye
 
Pole yake, kazidiwa sana.
 
Watanzania wanashangilia na kufurahia mtanzania mwenzao kapigwa kwenye ndondi. Safari bado refu
Mkuu watu wenyewe wakishapata umaarufu au pesa wanakua chawa wanaanza mambo ya asante mama sijui nini nini huku watu hatuna umeme hatuna ajira, mafuta na sukari vyote bei juu sasa kwanini tusishangilie na wao wakipoteza
 
Huyo mtasha amempiga ngumi za haraka haraka na za nguvu hadi Dullah Mbabe kushindwa kuendelea na pambano.

Wale ambao mmewahi kupigana,mnaweza kuwa mashahidi vile mtu huwa anajisikia akipigwa ngumi za usoni hasa kichwani

Yaani unaona nyota nyota tu 😜
 
Kama pesa sawa. Ila huko mbele hana viwango vyake. Dulla kwa sasa apambane na wahuni wenzake wa bongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…