Bondia Dullah Mbabe afanya mauaji kwa Ramadhan Migwede huko Masasi

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Juzi bondia Abdallah Pazi maarufu Dullah Mbabe alipata fursa ya kuandaliwa pambano na bondia chipukizi wa Masasi aitwae Ramadhan Migwede, Dullah alifanikiwa kushinda pambano hilo kwa knockout ya raundi ya 7 kati ya raundi 8 za pambano hilo.

Pamoja na kushinda, bondia Migwede alimmudu sana Dullah, alipelekeshana nae mwanzo mwisho hadi raundi ya saba ndipo Migwede aliposalimu amri kwa kubamizwa ngumi ya kichwa moja akaanguka chini na ndipo shughuli ilipokwisha.Kiukweli bondia Migwede ni chipukizi na Dullah yuko mikoa kusini ku promote ngumi baada ya kutoka Tunduru lakini pambano hili angedhalilika kama angefanya masihara maana Migwede alijitahidi sana kumkabili Dullah, changamoto kwake ilikuwa ni kukosa uzoefu.

Namshauri Dullah, pamoja na kuwa ndondo zinamuingizia kipato lkn kuna siku atamvagaa mbeba viazi ulingoni atamchukulia poa, ataumia, watu wanajua ngumi wanakosa promotion tu, halafu Dullah aongeze mazoezi, amekosa kabisa mbinu na fitness za kupambana, ukiliangalia pambano hilo kwenye YouTube huwezi amini kama anayepigana ni Dullah Mbabe.
 
Migwede kafa mmezika lini?
 
hayo mauaji yako wapi
 
Mtu anapigana vichochoroni huko halafu mnataka apigane na Mwakinyo
 
Kichwa cha Habari kimesheheni!!
 
Mleta mada hv unajua kama migwede anaishi Chanika na ni rafki wa dullah Mbabe yaani kfup ni majirani kabisa na wmekuja kupiga hela huko Masasi

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…