Bondia Floyd Mayweather amchakaza Conor McGregor kwa TKO ktk raundi ya 10

Jamaa wamepiga Bilion ngapi??


Unaambiwa McGregor ameingiza Bilioni 200.
Hapo alishaingiza hata kabla pambano kuanza.
Mayweather ndio usipime, maaana pambano lote limeingiza mapato zaidi ya Trilioni moja.
 
Ndindo ndio imekuamsha alfajiri! Wivu ni tabia za kishangingi! Floyd is a winner!
Pambano toka mwanzo lilikosa mvuto kila kitu kilikuwa kinajulikana ndio maana licha ya kiki nyingi ila imekuwa doro
 
Ndindo ndio imekuamsha alfajiri! Wivu ni tabia za kishangingi! Floyd is a winner!
Mkeo ndo kakwambia nimemuacha kitandani peke yake alfajiri? Mara ya mwisho nimeamka sababu ya ndondi ni enzi za Tyson, sijui unanielewa dogo??
Sijaangalia hilo pambano, alafu ina maana kutokuwa team ya mayweather ndo wivu? Mcgregor hakutakiwa kuwa na support??
 
Kumbe unaa admit kuwa lilikuwa pambano, sasa kwanini hutaki kukubali kuwa jamaa yako kapigwa!?
Hata Misosi FC walishinda PAMBANO la fainali ndondo, na ni wapi nimesema Mcgregor HAJAPIGWA? Naona wewe ndo uko infatuated na Mayweather kuliko uhalisia.
Una kichwa kizito, labda nikulainishie point yangu ni: Mayweather hastahili kuonekana kuwa ni genius wa boxing kupitia pambano hili, yuko vizuri ila sio kupitia pambano hili sababu aliyepigana nae sio BOXER.
 
Kwenye uzito wake ....huyu hapa aliyeshindikana ...View attachment 575774
Hapana, Antony Joshua ni heavyweight kama ilivyokuwa akina Mike Tyson, Mohamed Ali,Evander Holyfield na wengineo wakati Mayweather ni uzito mdogo tu, featherweight kama akina Cheka wa Morogoro.

Hivyo kumpiganisha Heavyweight kama Joshua na uzito mdogo kama Mayweather ni kesi ya mauaji, hairuhusiwi!

Hiyo itakuwa sawa na kumpiganisha mtoto wa miaka 8 na kijana wa miaka 25.
 
Inakuwaje mtu upo Temeke Mikoroshini unatokwa povu kuhusu watu waliopo Las Vegas?

Bora utokwe povu kuhusu Simba wa Tandale na Tembo maana wanatambua hata uwepo wetu.
 
Mkuu, kila mchezo una taratibu zake. Kwenye ngumi kinachogombewa huwa ni mkanda. Bondia akiwa na mkanda ina maana rank yake iko juu, akiwa ranked juu ina maana ana uhakika wa kupata kiasi kikubwa kuliko challenger yeyote atakayepambana naye kwa sababu atakuwa ranked chini yake. Kwa ishu ya Mayweather, hakukuwa na mkanda wowote officially lakini Mayweather alikuwa ranked juu kwa kuwa ana rekodi bora kuliko McGregor ambaye alikuwa hajawahi kupigana. Masuala ya malipo hujadiliwa kabla ya pambano na kila mtu anakuwa anajua atalipwa kiasi gani. Nadhani utakuwa umeelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…