Bondia Hassan Mwakinyo sasa ashika nafasi ya 86 duniani

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
April 2, 2020

Wachambuzi wa nyota ya Mwakinyo kufifia watoa sababu:

Mabondia walioitumikia Tanzania kwa muda mrefu na uzoefu wa kimataifa waelezea sababu ya ranking ya Hassan Mwakinyo kuporomoka toka nafasi ya 14 duniani kwenda nafasi ya chini ya 86 na changamoto zake.

Changamoto ni kuwa sasa Hassan Mwakinyo itakuwa vigumu kupata mapambano wenye mkwanja mrefu.

Wazoefu wamelaumu team yake, promoters, sponsors kwa kukosa ufahamu ya kumlinda na kumsaidia Hassan Mwakinyo kupakia angalau ktk 20 bora ulimwenguni ili walau ndoto ya kuwa bingwa wa ndondi wa uzito wake duniani itimie na pia kulipwa mapato na ufadhili / sponsorship zenye pesa nyingi.

Source:
Star TV habari

Marchi 27, 2019

Mwakinyo azungumzia mipango yake


Source: Clouds media
 
Lile pambano la uwanja wa taifa nadhani lilimuharibia pia.."makombe" na "hirizi" hayapigani uwanjani,yanakupa kujiamini kwa muda tu!
 
Mie toka alipoonesha ni mnazi wa CCM nkaona ndo mwisho kwa dogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna level fulani ukifikia kibongo bongo inakubidi tuu uwe mnazi wa CCM hata kinafiki ili mambo mengine yaende otherwise story zitakuwa tofauti kwako.

Tanzania sio Marekani.
 
Manager wake alieleza kwamba walishtushwa na hiyo ranking wakawasiliana na wanaohusika ranking wakasema wamekosea na kurekebisha,makosa hayo si kwa mwakinyo tu,kuna mabondia wengine wamewekwa juu hawana sifa na wengine wamewekwa chini hawana sifa hizo pia,manager wake alieleza kwamba hao wengi hawajapigana na mwakinyo amepigana Michezo mingi inakwaje awe chini.

Sasa sijui kama ni bla bla za wabongo au kweli
 
Hizo taarifa nilizisikia lakini wazungu wako makini sana kwenye hayo mambo si rahisi eti system nzima isigundue.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna level fulani ukifikia kibongo bongo inakubidi tuu uwe mnazi wa CCM hata kinafiki ili mambo mengine yaende otherwise story zitakuwa tofauti kwako.

Tanzania sio Marekani.
Huyu dogo nik mental case aisee nilimuona mjinga sana alipkuwa anaingia kwenye page ya kigogo 14 twitter na kuanza kutukanana naye hata kina mrisho mpoto hawajafikia hatua hiyo ,dogo ni limbukeni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…