Bondia Hemed Rashid apigwa hadi kutapika na kuzimia Dar Boxing Derby

Bondia Hemed Rashid apigwa hadi kutapika na kuzimia Dar Boxing Derby

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1669095231682.png
Bondia Hemed Rashid amepoteza pambano kwa TKO dhidi ya Iman Bariki 'Man Chuga', baada ya kupoteza fahamu na kupelekea kushindwa kuendelea na mapambano na kukimbizwa hospitalini kwa gari maalum ya wagongwa.

Bondia huyo alipoteza mchezo huo katika raundi ya nane katika pambano la Dar Boxing Derby, baada ya kupigwa ngumi za mfululizo na mpinzani wake huku akionekana kuchoka kabla ya mwamuzi kumaliza pambano. Hali iliopelekea kupelekwa kwenye kona yake kwa msaada kabla ya kuanza kutapika, hali iliopelekea daktari wa pambano Khadija Hamisi kuchukua uamuzi wa kumkimbiza Hospitali ya Temeke.

Pambano hilo lililopigwa kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam jana usiku. Mwandishi wa Nipashe leo amezungumza na daktari Khadija kuhusu hali ya bondia huyo na kueleza kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kumkimbiza kwenye hospitali ya Temeke, licha awali hali yake kuwa mbaya kutokana na kupoteza fahamu.

“Tunashukuru anaendelea vizuri kwa sababu amepatiwa matibabu na hadi sasa bado anaendelea na matibabu, lakini amefanikiwa kuamka na anaongea, alichokuwa analalamika sana ni maumivi ya kichwa, ingawa alitapika sana."

“Lakini amepewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Mwananyamala, ambapo tutampeleka kwa ajili ya kufanya vipimo vya CT Scan kwa kuangalia hali ya kichwa kipoje na vipimo ambavyo alifanya usiku baada ya kufika Temeke anaoneka yupo sawa. Isipokuwa hiyo CT Scan ambayo itafanyika leo,” amesema Dk. Khadija.
 
Ni jambo linaloweza kutokea muda wowote katika michezo hasa inayo husisha ngumi na mateke.
Tunamuombea Mwenyezi Mungu amjaalie Afya na arudi kuendelea na michezo pindi Afya yake ikitengemaa.
 
Huu mnaouita mchezo wa ndondi sijawahi kuukubali kabisa! Hivi kupigana ngumi unakuawaje mchezo?
 
Ndo matatizo ya kupigana ukiwa umelewa
 
Kuna sehemu kwenye mwili ukipigwa unatapika ulivyokula,vinatoka kama vilivyokua kabla ujavila.
 
Back
Top Bottom