John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
MANDONGA
Kwa sasa Nchini Tanzania ukitaja jina la MANDONGA watu wengi wataanza kucheka, hiyo ni kutokana na sifa za bondia huyo ambaye amejizolea umaarufu hivi karibuni hasa mwaka huu 2022.
MANDONGA amenikumbusha stori ya mtu anaitwa Felix KANYABOYA ambaye ndiyo huyo aliyesababisha neno KANYABOYA likazaliwa Nchini Tanzania, hiyo ni kwa kuwa sifa zao ni kama zinaendana.
Wote wawili ni mabondia maarufu kwa kupiga mikwara ya hatari, yaani kwa jinsi wanavyojisifia ni wazi kuwa kama mpinzani atakuwa mwepesi anaweza kujawa hofu, lakini wakishapanda ulingoni sasa ni burudani, kwa kuwa hawaoneshi kile walichokuwa wakitamba nacho.
Karim MANDONGA amekuwa maarufu kutokana na ile mikwara yake anayoonesha kabla ya pambano lakini mara mbili zilizopita alipopanda ulingoni alipata kipigo ambacho hakikuwa na ubishi kuwa kaonewa, bali ni kweli alizidiwa na akachapika Swadakta!
Julai 30, 2022 MANDONGA alichapika kwa TKO katika Raundi ya Nne dhidi ya Shaban Kaoneka lakini kabla ya pambano hilo, tambo na mikwara ya MANDONGA ilikuwa siyo ya Nchi hii.
Baada ya pambano hilo, imekuwa kama kichekesho nchini kila unapotaja jina la MANDONGA, watu wanaamini anafanana na KANYABOYA.
Nikukumbushe kidogo kuhusu KANYABOYA ambaye alikuwa ni bondia miaka ya 1980, huyu alivyokuwa na mikwara na kupata kichapo kila alippanda ulingoni tena mapema tu, watu wengi wakaanza kumfananisha mtu yeyote mwenye mikwara mingi sawa na KANYABOYA.
Yaani ikaonekana KANYABOYA ni mtu ambaye hawezi kufanya kitu cha maana zaidi ya mikwara au habari za uwongo uwongo
======================
Kanya Boya ni bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Burundi. Bondia huyu Felix Kanyaboya kati ya Miaka ya 1986 / 1987 alikuja kucheza Tanzania , Alikuwa anafikia Hotel za Kariakoo.
Bondia huyu alikuwa na Mikwara mingi saana na siku ya Mechi anatoka Hotelini Kariakoo anatembea kwa Miguu akiwa kavalia kabisa Gloves , ring bout, Gum shield, anapiga shadow box njia nzima na watu wanamshangilia mpaka Railways Club Gerezani. Akipanda Ulingoni Round zake 2 tu kapigwa KO mbaya na akina Habibu Kinyogoli, na Omary Yazidu. Ndipo Jina lake likavuma kama KANYABOYA NI KUMBUKUMBU TU Kutoka Maktaba.
Pia soma:
Bondia Mandoka achapika, Kidunda ashinda, Mapambano ya ndondi Songea, Julai 30, 2022
Mjue bondia KANYABOYA na mikwara yake, hadi neno la Kanyaboya likazaliwa kwa ajili yake