Bondia mrembo zaidi duniani Laila Ali

Bondia mrembo zaidi duniani Laila Ali

Mkuu kipindi mike tyson ametoka jela anaanza kupigana ulifatilia mapambano yake? Kama ulifatilia utakuwa ulimuona huyu maana kwenye mapambano ya utangulizi alikuwepo, tatizo la huyu demu anapiga kama wanaume
Hahahahah anakupa nako mpaka unasema uwii nisamehe mke wangu utaniua baba watoto wako sichelewi kurudi tena 😂😂😂
 
Bondia Laila Amaria Ali ni mtoto wa nane kati ya tisa wa Bondia Muhammad Ali, mwanadada huyu anatajwa kama ‘Bondia Mrembo zaidi Duniani’. Kwa sasa ameshastaafu mchezo huo wapili kwa kupendwa zaidi Tanzania baada ya Mpira wa miguu, akiwa ameanza mapambano mwaka 1999 mpaka 2007.

Laila.jpeg


Katika mapambano yake hajapoteza hata moja mpaka anatundika ‘gloves’, katika mapigano 24 aliyoshinda, 21 amewadondosha wapinzani wake kwa KO. Kwa sasa ana umri wa miaka 43 bondia huyu wazamani wa Marekani.

0615_oag-laila-ali-1000x813-1.jpeg


2012 ameshinda tuzo ya AOC, 2002, 2005, 2007 WBC WIBA World Super Middleweight, 2004 IWBF Female light heavyweight na 2002-2004 IWBF & IBA female Super Middleweight. Kwa kifupi hakubakiza kitu kwenye kila mkanda aliyopigania mwanadada huyu ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 43 akionekana mwenyefuraha tele kwenye maisha yake.


g252145_u95731_images_1.jpeg


Waswahili wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka, huyu aliamua kutembea mulemule alipopita baba yake Muhammad Ali wapenzi wa ngumi hakuna asiyemjua, katika zama zake alifanya makubwa. Dunia inamtambua Laila Ali kama moja kati ya Bondia wa kike wakubwa wa muda wote.
Msitukhanithi enyi watu.

Kwa urembo sawa lakini sio kuitia hiyo "zaidi duniani"

Labda ungesema "mrembo zaidi duniani kwa muono wangu"
 
Mkuu kipindi mike tyson ametoka jela anaanza kupigana ulifatilia mapambano yake? Kama ulifatilia utakuwa ulimuona huyu maana kwenye mapambano ya utangulizi alikuwepo, tatizo la huyu demu anapiga kama wanaume
Kama Mwanaume
 
The game aliwahi kurap “Got a bitch that look like Laila Ali sittin' in my lap”
 
Kwa bongo tunao wanawake wanaocheza hiyo boxing? Nahitaji niwaone
 
Back
Top Bottom