Kaka
JF-Expert Member
- Nov 22, 2006
- 745
- 372
Bondia Ibrahim Class Mgendera (26) almaarufu “King Class Mawe” amefanikiwa kutwaa mkanda wa ubingwa wa wa uzito wa kati (lightweight) unaotolewa na Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council) kwa kumpiga bondia Jose Forero almaarufu kama “chui” kutoka katika pambano la mizunguko 12.
Pambano hilo lilichezwa siku ya Jumamosi, tarehe 1 Julai, 2017 katika ukumbi wa Müggelspree, Hangelsberg, Brandenburg nchini Ujerumani na kushuhudiwa na zaidi ya mashabiki mia tano wengi wao wakiwa ni raia wa nchi mbalimbali za ulaya na wachache kutoka nchi za Afrika. Ibrahim kabla ya kupanda ulingoni na huku akijiamini sana aliwahakikishia Watanzania kwamba ataibuka na ushindi na kunyakua mkanda huo na kwa mikono yake angependa kumkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuli mara atakaporejea nyumbani.
Mchezo ulianza kwa Ibrahim kurusha makonde mfulululizo kwa mpinzani wake ambaye naye alijitahidi kuwa imara zaidi huku akipata kuungwa mkono zaidi na mashabiki wengi wa waliohudhuria pambano hilo. Hali hiyo haimkumkatisha tamaa Ibrahim kuendelea kupamba zaidi ambapo mpaka pambano linafikia mzunguko wa 12 ambao ndio wa mwisho Ibrahim alionekana bado ana nguvu ya kuendelea na pambano hilo. Majaji wote watatu katika pambano hilo walimpa Ibrahim ushindi wa 120-108, 119-109 na 118-110 dhidi ya mpinzani wake na hivyo kukabidhiwa mkanda huo wa ubingwa.
Ushindi huo umemuwezesha Ibrahim kuongoza orodha ya mabondia bora katika uzito wake nchini huku akiwa nafasi ya tisa kwa bara la Afrika na 114 kwa dunia nzima kwa mujibu wa tovuti ya Boxrec wakati huo huo Baraza la ngumi duniani (GBC) likimpa nafasi ya tatu na kabla ya ushindi huo hakutambuliwa katika orodha yake ya mabondia bora.
Meneja wa Ibrahim Bi. Victoria Joseph ambaye pia aliambatana naye huko Ujerumani pamoja na kiongozi wa Kamisheni ya Ngumi za KUlipwa Tanzania (TPBC) ndugu Joe Joseph, aliupokea ushindi huo kwa furaha sana na kuahidi kuendelea na hatua inayofuata katika kumuandaa bondia wake kwa ajili ya kuutetea mkanda huo ambapo GBC walitoa fursa kwa Tanzania kupewa kipaumbele cha kuwa mwenyeji wa pambano hilo la marudiano huku Panama na Marekani zikipendekezwa pia endapo Tanzania haitoweza kuandaa pambano hilo.
Kaka ...